Na Gideon Gregory, Dodoma.
Serikali imezindua
mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye
mikuza inayotumiwa na taasisi na kampuni za huduma mbalimbali lengo likiwa ni kuimarisha
usalama wa umma, kuongeza uadilifu na usimamizi makini wa miundombinu iliyopo
chini ya ardhi,
Akizungumza wakati
wa uzinduzi huo kwa niaba ya katibu mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Kamishna
wa Petroli na Gesi Asilia kutoka Wizara
ya Nishati, Mhandisi Michael Mjinja amesema kuwa mwongozo huo utasaidia katika kuimarisha usalama na kuwa
na usimamizi makiji kwenye miundombinu iliyopo chini ya ardhi.
Amesema kuwa usimamizi
wa pamoja
wa Miundombinu Iliyoko Chini ya Ardhi Kwenye Mikuza (wayleave) wa Mwaka 2023,
unazinduliwa kwa
dhumuni la kuimarisha usalama wa umma, kuongeza uadilifu
na usimamizi makini wa miundombinu iliyopo chini ya ardhi Tanzania Bara.
“Mwongozo huu utasaidia katika kuratibu shughuli za ujenzi, uendeshaji, marekebisho na matumizi mengineyo ya mikuza inayotumiwa kwa pamoja na wadau mbalimbali bila kuathiri usalama wa miundombinu, umma na mali zao.” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dk. James Andilile amesema kuwa mamlaka hiyo imeratibu zoezi la uandaaji wa mwongozo huo kuanzia mwaka 2019 pamoja na timu za Wataalamu kutoka kwa wamiliki na watumiaji wa Mikuza na Wakuu wa Taasisi kwa kuridhia mwongozo huo.
Dkt. Andilile amesema
kuwa miaka ya hivi karibuni usambazaji wa gesi
asilia katika miji ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara umeongezeka.
Ongezeko hilo
limepelekea shughuli za utandazaji wa
miundombinu katika mikuza inayotumiwa na watoa huduma mbalimbali, yakiwemo
mabomba ya usambazaji wa mafuta
na maji, miundombinu ya umeme na mawasiliano.
“Shughuli
za uchimbaji ili kutandaza miundombinu kwenye mikuza haziepukiki kwani mahitaji ya huduma
zinazotolewa na kampuni mbalimbali zinazidi kuongezeka na kufanyika bila ya
kuratibiwa; hivyo basi kusababisha uharibifu wa miundombinu iliyofukiwa chini
ya ardhi, migogoro na kuhatarisha usalama
wa miundombinu hiyo, watu na mali zao.” amesema.
Amesema kuwa kukosekana kuratibiwa kwa shughuli hizi,
zinatokana na mikuza hiyo
kumilikiwa na taasisi tofauti na zile zinazotoa huduma
katika mikuza hiyo. Mikuza yenye muingiliano mkubwa wa miundombinuni.
Amesema kuwa baada ya maandalizi ya muda mrefu, timu ya wataalamu imekamilisha maandalizi ya mwongozo huo na rasimu ya mwongozo ilipitiwa na wamiliki na watumiaji wa mikuza. Mwongozo huu utaratibu shughuli za ujenzi, uendeshaji, marekebisho na matumizi mengineyo ya mikuza
“Tunaamini
wamiliki na watumiaji, wataufuata mwongozo huu katika utumiaji wa mikuza ili
kulinda miundombinu hiyo, kuepusha migogoro na kuokoa maisha ya watu na mali
zao,” amesema.
Naye mwenyekiti wa
kamati ya ya bodi ya nishati, Haruna
Masebu alisema kuwa kumekua
na ongezeko la shughuli zisizoratibiwa
kwa pamoja katika utaratibu usio rasmi
kwenye miundombinu iliyoko chini ya ardhi.
“Hali hii
imepelekea athari kubwa za kiusalama, uharibifu wa mali, mazingira na ajali kwa
watu, mfano ni ajali za kupasuliwa kwa mabomba ya gesi asilia, mafuta na maji
wakati wa shughuli za ujenzi na maboresho ya miundombinu katika maeneo mbali
mbali” alisema
Amesema kuwa makubaliano
haya yalihusisha Taasisi na kampuni zifuatazo TAZARA, TAZAMA, SONGAS, TPDC,
GASCO, TRC, TTCL, M&P LIMITED, TANROADS, PAET, TANESCO, DAWASA na TARURA.
Ameongeza kuwa juhudi hizo hazijafikia Taasisi na Kampuni zote zenye miundombinu chini ya ardhi kwa mfano mamlaka za maji mikoani, kampuni za mawasiliano na kampuni za madini.