Makumi ya wananchi wa Morocco wameandamana katika mji mkuu Rabat na kutangaza kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Isarel.
Waandamanaji hao walisikika pia wakipiga nara za kulaani mashambulio ya anga ya jeshi la Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na wakkatii huo huo kutangaza kuwa pamoja na wananchi hao wa Palestina.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba bendera za Palestina wametangaza kuwa, wanapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Iisrael kwa namna yoyote ile.
Wananchi wa Morocco hadi sasa wameshaandamana na kumiminika mabarabarani mara kadha wa kadha sambamba na kuzichoma moto bendera za utawala haramu wa Kizayuni kuonyesha upinzani wao dhidi ya hatua ya serikali ya Rabat kuanzisha uhusiano wa kawaida na Tel Aviv na kutaka uhusiano huo ukomeshwe.
Hivi karibuni pia, baadhi ya wabunge wa Bunge la Morocco wamebainisha upinzani wao kwa hatua ya kuanzishwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na wakatangaza kuwa kuanzisha uhusiano na utawala huo kutakuwa sawa na kupuuza mapambano ya watu wa Palestina na haki yao ya kuunda nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa ni Baitul Muqaddas.
Desemba 2020, Morocco na utawala haramu wa Israel zilifikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida kwa ushawishi wa Marekani. Na kama sehemu ya makubaliano hayo, Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump alikubali kutambua mamlaka ya Morocco juu ya Sahara Magharibi. Hata hivyo serikali ya rais wa sasa wa nchi hiyo Joe Biden imesema itauangalia upya uamuzi huo.
Chanzo #Parstoday.