TRA yazindua kampeni ya Tuwajibike:

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Emmanuel Kawau.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Imezindua rasmi leo Mei 2/ 2023 kampeni inayojulikana kwa jina la  "Tuwajibike" inayolenga kuwakumbusha na kuwahamasisha wauzaji wa bidhaa na wananunuzi kutoa na kudai risiti halali za EFD.



Akizungumza wakati akitambulisha kampeni hiyo kwa waandishi wa habari Mkurugenzi wa Idara ya huduma na Elimu kwa mlipakodi Richard Kayombo amesema Tuwajibike ni kampeni yenye malengo makuu  matatu ikiwemo kuwakumbusha na kuwahamasisha wauzaji wa bidhaa na watoa huduma nchi nzima kuwajibika kwa kutoa risiti halali za EFD kila wauzapo bidhaa au kutoa huduma.


Kampeni pia imelenga kuwakumbusha na kuwahamasisha wanunuzi wa bidhaa na huduma kote nchini kuwajibika kudai risiti halali za EFD pamoja na kuzikagua ili kujiridhisha kuwa inakidhi vigezo vyote muhimu kadhilika kampeni  itahusisha kufuatilia utoaji wa risiti halali za EFD nchi nzima pamoja na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofuata sheria katika utoaji wa risiti.

" Risiti halali za EFD zinatakiwa kukidhi vigezo vikuu vinne (4) ambavyo ni jina la biashara,tarehe halisi ya mauzo,kiasi halisi cha pesa kilichonunuliwa bidhaa au TIN ya mnunuzi au vyote kwa pamoja" Alisema kayombo.

Aidha TRA inasisitiza kuwa adhabu kali itachukuliwa kwa yoyote atakayebainika kufanya udanganyifu ambapo kwa mfanyabiasha atakayebainika kutokutoa risiti halali ya EFD au kufanya udanganyifu atatozwa faini ya Shilingi 3,000,000/= mpaka Shilingi 4,500,000/= au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

"Na kwa mnunuzi atakayebainika kufanya manunuzi bila ya kudai risiti halali za EFD atatozwa faini ya Shilingi Elfu 30,000/= mpaka  shilingi Milioni moja na laki tano"

"TRA Tunapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara wote kuwajibika kwa kutoa risiti halali za EFD bila ya kushurutishwa na wanunuzi kudai risiti halali za EFD kwa kila manunuzi watakayoyafanya ili kuepuka usumbufu usio wa lazima na wakati huo huo kuisaidia serikali kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo na kukuza uchumi wa nchi nzima" Alisisitiza Richard

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)