Ameeleza hayo Mei 06, 2023 wakati akiongea na wananchi wa Kegonga na Kwihancha wilayani Tarime alipoambata na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeo ya Makazi na Naibu Waziri Maliasili na Utalii kukutana na wananchi ili kutoa elimu, kukagua mipaka na kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo katika vijijiji husika.
“Serikali haijabadilisha mipaka wala haijaweka alama mpya nyingine tofauti na zilizokuwepo awali kulingana tangazo la Serikali namba 235 la mwaka 1968, kilichofanyika ni kuweka alama za kudumu kwa kutafsiri kile ambacho tangazo na sheria inavyoelekeza” amesema Waziri Kairuki
Waziri Kairuki ameomgeza, Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia wataalam wa kusoma ramani kwa kutoa tafsiri zaidi juu ya alama za mipaka zilizowekwa ili kuonesha maeneo ya mipaka na maeneo ya shughuli za uhifadhi.
Aidha, Waziri Kairuki ameiagiza Halmashauri ya Wilaya Tarime kwa kushirikiana na Tume ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi kukamilisha mpango wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo ambalo lilikuwa limewekewa alama hizo ikiwa ni pamoja na eneo la mita 500 ambazo zimetolewa kwa wananchi kufanya shughuli zinazoendana na uhifadhi.
Waziri Kairuki amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ruhusa kwa wananchi waliolima mazao, kuvuna mazao yao pindi yatakapokomaa lakini hawataruhusiwa kulima katika maneo ya ndani ya mipaka ya hifadhi ya Serengeti ambayo yamewekewa alama kwa mujibu wa Sheria.
“Ramani ya mipaka italetwa kwa wananchi ikiwa imetafsiriwa kwa kishwahili ili mzidi kupata uelewa elimu zaidi ya alama za mipaka, kikubwa zaidi tuendelee kuheshimu kile ambacho kimetolewa kwenye Tangazo na kuheshimu wataalam” amesema Kairuki
Ziara hiyo ya timu ya Mawaziri watatu ya ukaguzi wa alama za mipaka ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu kwa timu ya Mawaziri hao kwenda kwenye vijiji husika vyenye migogoro katika Wilaya za Tarime na Serengeti kwa lengo la kukutana na wananchi ili kutoa elimu, ufafanuzi na kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo katika vijijiji husika.

