NMT YAWA DARASA LA AMANI KWA WATALII KUTOKA MAREKANI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Amani iliyopo Tanzania  imeendelea kuwa kichocheo kikubwa cha Watalii kumiminika nchini ambapo watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekuwa mbali ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini Makumbusho ya Taifa (NMT)  imekuwa ndio sehemu muhimu ya  kuitembelea  kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali hususan historia, Chimbuko la mwanadamu, Mila na Desturi pamoja na Onesho la Matumaini baada ya Huzuni.


Akizungumza kwenye ziara ya kimasomo ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Georgia cha nchini Marekani kwenye Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Mkufunzi wa Chuo hicho, Dkt. McMurray amesema uamuzi wao wa kuitembelea Makumbusho hiyo ni kutokana na utajiri wa taarifa muhimu hususan zinazohusu amani zilizohifadhiwa na kuoneshwa kwenye Makumbusho ya Taifa.


Dkt. McMurray ameongeza kuwa, wanachuo wengi katika Chuo hicho wamezaliwa miaka ya 2000 baada ya tukio la Kigaidi la Bomu katika Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam na Nairobi nchini Kenya Mwaka 1998 hivyo Onesho la "Matumaini baada ya Huzuni" lililopo NMT ni darasa la kuwafundisha kuhusu  umuhimu wa amani.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)