Hapo pichani chini ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb) akisalimiana na wananchi wa kata ya Dabalo wakati alipowasili katika hafla ya makabidhiano ya Jengo la Upasuaji, Wodi ya Wazazi, Vifaa, vifaa tiba na gari la kubebea Wagojwa katika katika kituo cha afya Dabalo. Leo tarehe 09 Mei 2023.
Makabidhiano yatafanyika kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kupitia mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi, watoto na vijana (RMNCAH - UNFPA) iliyofadhiliwa Serikali ya Denmark ambapo Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki.