MWONGOZO WA KUIMARISHA MAZINGIRA YA WAFANYABIASHA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Mkurugenzi wa uwezeshaji wananchi kiuchumi na maendeleo ya sekta binafsi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Conrad Milinga amesema kuwa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji inaandaa mwongozo wa kuwawezesha wafanyabishara wajasiliamari kujiimarisha zaidi kiuchumi.


Milingi ameyasema hayo Mei 16,2023 Jijini Dodoma, katika kikao cha kuthibitisha rasimu ya muongozo wa wataalamu wa biashara na mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (MKUMBI).


Amesema wanahitaji kuandaa huo muongozo ili watu wajue wapi pa kuanzia na utekelezaji wake utakuwa mkubwa.

“Sasa hivi unakuta mtu anataka kusajiri biashara yake anaenda Brela anaambiwa nenda kwingine, sasa kumbe kama angelikuwa amepata zile taarifa kuanzia mwanzoni anakuwa anajua akitaka kufanya kitu hiki ni nani nan ani anahusika na kwa garama gani,”amesema. 


Aidha amesema kuhusiana na taarifa za mwenendo wa bei za vyakula nchini wanahitaji kuzipata kuanzia kwao lakini zisitofautiane na zile zinazotolewa na wizara, hivyo waweke mfumo wa taarifa watakazo kuwa wanazipata kutoka kwao.

Amesema hawataki suala la kwenda jiji kukusanya mapato ambayo hawajui yanatokea wapi, lazima watengeneze watu watakao wapatia mapato.

“Hatutaki suala la kuhamka asubuhi na kwenda kumfungia mtu bishara yake, tunataka tumjengee uwezo ili ajue ana wajibu gani, sisi tuna wajibu kwenye biashara na yeye anawajibu wa gani katika kuchangia mapato ya serikali, kwahiyo yasiwe mambo ya kusukumana,”amesema.


Kwa upande wake katibu tawara masidizi wa viwanda, biashara na uwekezaji mkoa wa Kigoma Degratias Sangu, amesema kabla ya kuanzishwa kwa idara hiyo wizara ilikuwa ikifanya, kuunda, kupendekeza pamoja na kuanzisha sera ambapo utekelezaji wa chini haukuwa thabiti kwasababu haukuwa na wasimamizi, hivyo kupitia idara hiyo wasimamizi wana mwendelezo wa majukumu yaliyopangwa yatatimizwa.


Amesema katika kutimiza majukumu ambayo wamekuwa wakiyafanya Pamoja na wafanya biashara mtazamo na dhana kamili ya kufanya mahusiano mazuri na maafisa wenye damana ya kusimamia unakuwa chanya na kuwaona sio maadau.

“Isifike mahara fulani mfanya biashara akimuona afisa biashara akakimbia akajua huyu sio anakuja kunisaidia, anakuja kunifungia biashara au kuniongezea vitu tofauti kwahiyo kupitia vikao kama hivi na semina kama hizi kwakweli zinatusaidia na sio tunarudi kama tulivyokuja tunarudi na mtazamo mpya na mzuri wa kufanya kazi kwa pamoja na hawa ambao wanalipa kodi,”amesema.


Naye katibu tawala msaidizi viwanda, bishara na uwekezaji mkoa wa Morogoro Beatrice Njawa amesema kwakuwa wamepitishwa kwenye mpango wa kuboresha mazingira ya kufanyia bishara anaamini wanaenda kusimamia na kuondoa vikwazo vyote vya kibishara na uwekezaji katika mamlaka za serikali za mitaa na mikoani ili kuweza kutangaza uwekezaji unaopatikana katika maeneo hayo.


Njawa ameongeza kuwa wakiweza kuboresha eneo hilo hasa uwekezaji na ujenzi wa viwanda maana yake wanaenda kuzipa nguvu mamlaka za serikali za mitaa na wataongeza mapato na wanaenda kuimalisha mahusiano kati ya mikoa, halmashauri pamoja na sekta binafsi zilizopo katika maeneo yao.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)