WAFANYABIASHARA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ADHIMU KATIKA SOKO HURU LA AfCFTA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Lugano Wilson awahimiza wafanyabiashara kuchangamkia fursa adhimu katika eneo la soko huru la Biashara Afica - African Continental Free Trade Area (AfCFTA) ili kuongeza uzalishaji na uongezaji wa thamani kwenye mazao ya mifugo na uvuvi.


Dkt Lugano ameyasema hayo tarehe 13 Aprili,2023 katika ukumbi wa hoteli ya Dodoma wakati akitoa mada kwenye ufunguzi wa kongamano la wadau wa sekta ya kilimo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah.

Kongamano hilo la tisa kufanyika linahusisha wadau wa sekta ya kilimo ili kufanya tathimini ya matokeo ya tafiti na maboresho ya sera, kanuni na sheria katika sekta ya kilimo ili kuweka mazingira wezeshi yatakayoleta mageuzi katika sekta ya kilimo na mnyororo wa thamani pindi utekelezaji wake utakapoanza.

Aidha akizungumza katika kongamano hilo Dkt. Lugano amewaomba wafanyabiashara waliotayari kufanya biashara katika eneo la soko huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kutumia fursa ya soko hilo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na uchumi wa wafanyabishara wetu.

“Katika kujipanga Serikali kwa sasa inaendelea kukamilisha mkakati wa kitaifa wa utekelezaji wa mkataba wa (AfCFTA), wataalam wa wizara wapo Dar es Salaam wakishirikiana na sekta binafsi kwa lengo la kuweka mikakati bora na endelevu ya kuwezesha nchi yetu" Amesema” Dkt Lugano.

Dkt. Lugano ameongeza kuwa mapendekezo yatakayotolewa katika mkutano huo yatakuwa na tija kubwa hivyo tuwaombe wadau wa biashara walio tayari kufanya biashara chini ya AfCFTA wasisite kutuona ili tuweze kuwaunganisha katika programu zinazoendea.

Dkt. Lugano ameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi saba ambazo zimeridhia mkataba huo na kuwa miongoni mwa nchi za awali ambazo zitanufaika kupitia programu iliyoanzishwa na sekretarieti ya AFCFTA.
Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)