KAMPUNI YA MKWAWA YATOA MSAADA KWA WAHITAJI TABORA

MUUNGANO   MEDIA
0

Kampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku ya Mkwawa Tobacco Leaf mkoani Tabora limetoa vifaa mbalimbali na sadaka kwa vituo viwili vya watoto yatima na Magereza vitu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 20,445,000/.

Akizungumza wakati wa utoaji wa vifaa hivyo na sadaka hiyo mkurungezi mkuu wa kamapuni hiyo Matthew Kapnias alisema kwamba wametoa kwa ajili ya watu wenye uhitaji iliiweze kuwasaidia katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema kwamba uongozi wa kampuni hiyo uliona kuna umuhmu wa kufanya hivyo kwa vikundi hivyo na kuisaidia serikali kuwapatia sadaka kwa wahitaji waliomo  kwenye taasisi hizo za kijamii.

Alitaja vitu vilivyotolewa ni Mchele kilo 3000,Sukari mifuko 50,Mafuta ndoo 20,Sabuni katoni 50, Karanga kilo 125 na wembe dazani 400.

Alivuitaji vitu vingine kuwa ni Magodoro 115 ,Mashuka 280 Na Neti 185.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)