Katika Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika Wilaya ya Kyerwa, kata ya Mabira viwanja vya shule ya Sekondari Mabira, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila ametoa elimu juu ya ugonjwa wa Marburg na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.
Aidha, amewasihi wananchi kutowanyanyapaa wagonjwa na wahisiwa kwani wagonjwa waliopona wamethibitishwa kuwa wazima na hawana maambukizi ya virus vya Marburg.
Halikadhalika amemshukuru sana Mheshimiwa Rais kupitia Wizara ya Afya na wadau wote waliofika Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kudhibiti maambukizi mapya na mpaka sasa Mkoa upo salama hivyo wananchi waendelee na shughuli zao huku wakichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu.
Wananchi takribani 4,000 wamepata elimu hiyo.