Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *CPA, Amos Makalla* amepiga marufuku utaratibu wa wafanyabiashara *kuuza bidhaa kwa kuzipanga chini* hususani *bidhaa za chakula* kwakuwa ni hatari kiafya hasa msimu huu wa *mvua* ambapo kunaweza kutokea *magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.*
*RC Makalla* ametoa onyo Hilo wakati wa *zoezi la usafi wa pamoja* soko la Machinga complex ambapo amewaelekeza *Viongozi wa masoko yote kudhibiti na kusimamia agizo Hilo.*
Aidha *RC Makalla* ametumia zoezi Hilo kuwahakikishia *wafanyabiashara waliokuwa soko la kariakoo* kuwa ujenzi ukikamilika *kipaombele kitakuwa kwa wale waliokuwepo awali.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* ameendelea kupiga *marufuku ufanyaji biashara kwenye Maeneo yaliyokatazwa* na kuwataka kwenda kwenye masoko rasmi Ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali hususani mikopo.
*CPA Makalla* pia ameelekeza *Kila mtendaji kwenye eneo lake kuhakikisha anasimamia zoezi la usafi* na kubainisha kuwa watakaoonekana kulegalega watachukuliwa hatua.
