PUTIN ATEMBELEA MAENEO YA VITA LUHANSK NA KHERSON, UKRAINE.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Rais wa Russia, Vladimir Putin, amefanya ziara ya ghafla ya kutembelea maeneo ya vita ya Luhansk na Kherson katika hatua ambayo haikupangwa hapo awali.

Ripoti zinasema Jumanne ya leo, Rais wa Russia amekutana na wanachama wa kundi la kijeshi la "Dnepr" alipokuwa akizuru eneo la Kherson, na kisha akakutana na askari wa Gadi ya Kitaifa "Vostok" wakati wa ziara yake katika mkoa wa Luhansk. 

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na Putin katika maeneo haya ya vita, na kulingana na Idara ya Vyombo vya Habari ya Ikulu ya Rais wa Russia, hakuna maandalizi yoyote yaliyokuwa yamefanywa kwa ajili yake.

Katika mazungumzo yake na makamanda wa kijeshi wa mikoa hiyo miwili, Rais wa Russia alifahamishwa kuhusu mwenendo wa vita kwenye maeneo hayo.

Mwezi Machi mwaka huu pia, Putin alitembelea mkoa wa Mariupol ambako pamoja na kutathmini kwa kina miundombinu ya eneo hilo, alikutana na kufanya mazungumzo na wakaazi wa eneo hili.

Februari 21, 2022, Rais wa Russia alikosoa mienendo ya nchi za Magharibi ya kupuuza wasiwasi wa usalama wa Moscow na akatangaza kutambua rasmi uhuru wa Jamhuri za Watu wa Donetsk na Luhansk katika mkoa wa Donbas huko Ukraine.

Siku tatu baadaye, Februari 24, 2022, Putin alianzisha operesheni "maalumu ya kijeshi" dhidi ya Ukraine, na vita baina ya pande hizo mbili bado vinaendelea.

Chanzo #Parstoday

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)