Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya Ghana kuwa nchi ya kwanza duniani kuidhinisha chanjo hiyo ya (R21).
Mkuu wa Wakala wa Kitaifa wa Kusimamia na Kudhibiti Chakula na Dawa nchini Nigeria, Mojisola Adeyeye, amesema chanjo hiyo itatumika kuzuia ugonjwa wa malaria kwa watoto wenye umri wa kati ya miezi mitano na miaka mitatu kwa kundi lililo hatarini zaidi.
NAFDAC imesema chanjo ya R21 ya Taasisi ya Serum nchini India inakidhi vigezo vya usalama na ufanisi baada ya tathmini ya Kamati ya Pamoja ya Mapitio.
Kamati ya mapitio ilibainisha kuwa chanjo hiyo ina ufanisi wa asilimia 75 katika kutoa kinga dhidi ya malaria.
Nigeria ina idadi kubwa zaidi ya vifo vya malaria duniani kote.
Baada ya Nigeria nchi ya Afrika Kaskazini, Algeria, pia jana ilitoa kibali cha matumizi ya chanjo hiyo kwa watoto wake.
Malaria inaua zaidi kuliko COVID-19 barani Afrika. Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa mwaka 2019 malaria iliua Waafrika 386,000.