Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu (Kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi Bw. Athumani Masasi kuhusu hatua ya ujenzi wa jengo la huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bahi jana tarehe 13/04/2023. Halmashauri ya Wilaya ya Bahi iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa majengo 18 kati ya majengo 28 yanayotakiwa kwenye hospitali hiyo jumla ya Shilingi Bilioni 4.3 zimetumika.
Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Honest Kasasa wa Hospitali ya Wilaya ya Bahi kuhusu huduma zilizoanza kutolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Bahi jana tarehe 13/04/2023.
Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu (Kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi Bw. Athumani Masasi mara baada ya kufanya
ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Ujenzi wa Zahanati ya
Nagulo Bahi ambapo ujenzi wake uko katika hatua za umaliziaji. Kituo hiki ni jitahada
za wananchi waliohamasishana kuanza ujenzi mwaka 2019 na kuungwa mkono na
Halmashauri ya Bahi.
Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu akikagua ujenzi wa madarasa katika
Shule ya Msingi Mpamantwa Barabarani ambapo ujenzi wake umekamilika ikiwa ni
jitihada za wananchi na Serikali ya Kijiji ambapo ujenzi wake umegharimu kiasi cha
Shilingi 38,893,980/=
Na Mwandishi Wetu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amesema lengo na matarijio ya
Mkoa nikuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia muda
uliowekwa na viwango vya ubora unaotakiwa kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Gugu ameyasema hayo leo tarehe 13/04/2023 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya
katika Wilaya ya Bahi kwa lengo la kukagua utekezaji wa miradi ya maendeleo
katika wilaya hiyo.
Gugu amehimiza watumishi wanaosimamia miradi hiyo kuwajibika na kuhakikisha
usimamizi madhubuti wa miradi yote ya maendeleo na kutoa angalizo juu ya hatua
zitakazochukuliwa dhidi ya miradi ambayo haitakamika kwa wakati na ubora
unaotakiwa.
“Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi
ya afya na elimu katika Halmashauri zetu, tusiwe moja ya vikwazo katika kusimamia
ukamilifu wa miradi hii, tunatoyaka kufanya yafanyike kwa wakati na hapa nisisitize
kubwa zaidi kusiwe na viporo vya kutokamilika kwa miradi ya maendeleo. Sote
tudhamirie kukamilisha kazi zote zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa
fedha kwa kuzingatia mpango kazi” Gugu alisisitiza.
Awali, Katibu Tawala Bw. Gugu alipata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa
Wilaya ya Bahi na kuwataka kutumiza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na
Kanuni za Utumishi wa Umma.
“Haki zinaenda sambamba na wajibu, hivyo timizeni wajibu wenu kikamilifu kila
mmoja katika nafasi yake”
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa
majengo 18 kati ya majengo 28 yanayotakiwa kwenye hospitali ya Wilaya ambapo
jumla ya Shilingi Bilioni 4.3 zimetumika.
Kutokana na kukamilika kwa baadhi ya majengo katika Hospitali hiyo imewezesha
kuanzishwa kwa huduma ya mionzi, huduma ya upasuaji ambapo mpaka sasa akina
mama 212 wamefanyiwa upasuaji, uwepo wa huduma za X-Ray na Ultrasound na
kutoa huduma kwa watoto waliozaliwa chini ya umri kamili wa mimba yaani Watoto
njiti.
Bw. Gugu katika ziara yake amekagua pia ujenzi wa Zahanati ya Nagulo, Shule ya
Msingi Bahi English Medium Pre and Primary School, Shule ya Msingi Mpamantwa
Barabarani na Shule ya Msingi Kigwe yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu.