MAADHIMISHO YA USALAMA WA AFYA MAHALA PA KAZI KITAIFA KUFANYIKA MOROGORO.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof Joyce Ndalichako amesema kuwa takwimu zilizofanywa mwaka 2021 zinaonesha jumla ya watu milioni 2.9 hupoteza maisha duniani wakiwa katika mazingira ya kazini na jumla ya watu milioni 402 duniani hupata ajali wakiwa katika mazingira ya kazini.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo Aprili 26 ,2023 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kilele cha maadhimisho ya Usalama wa Afya mahala pa kazi yatakayofanyika kitaifa mkoani Morogoro.

Amesema kuwa kwa takwimu za Nchini Tanzania zinazoishia Julai mwaka 2019 hadi 2022 jumla ya magonjwa katika maeneo ya kazi ni 4993 ambapo ajali ni 247 na vifo ni 217.

“Maadhimisho haya hapa Tanzania ni ya 19 na kitaifa yatafanyika mjini Morogoro ambapo yanaanza rasmi leo Aprili 26 na kilele kitakuwa tarehe 28 Aprili na wakati huo sikukuu ya wafanyakazi nchini kitaifa itakuwa hapo hapo Morogoro,”amesema.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa usalama mahali pa kazi na mazingira ya kazi serikali imekuwa ikishirikiana na OSHA kuhakikisha mazingira ya kazi kwa watumishiwa sekta zote wanafanya kazi kwa mazingira ambayo ni salama kwa afya zao.

Aidha, amewataka watumishi kuhakikisha wanapokuwa wakisafiri kikazi kuhakikisha wanatoa taarifa ili inapotokea ajali au kifo iwe raisi kuwatambua na kuwa tayari wapo katika mfuko wa fidia jambo ambalo ni muhimu kulizingatia.

“Sehemu kubwa ya uzalishaji kwa maana ya viwanda kunaongoza ambapo kunachangia kwa kiasi kikubwa katika kusababisha ajali kutokana na kuwa vijana wengi wasiokuwa na uzoefu hufanya kazi katika viwanda hivyo na Mazingira magumu sana,”amesema.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi, Hadija Mwenda amesema kuwa kutokana na utafiti mdogo walioufanya wamebaini ajali nyingi kazini zimekuwa zikitokea katika Sekta ya uzalishaji kwa maana ya Viwanda huku akieleza hatua ambazo wameanza kuchukua.

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA)Tumaini Nyamhokya ameiomba Serikali kuweka Sheria kali ambazo zitawabana Waajiri kuzingatia masuala ya usalama mahala pa kazi.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)