Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI
WIZARA 12 za Kisekta zimewapitisha Wakuu wa Wilaya kwenye vipaumbele vya Wizara zao ili kuwajengea uelewa utakaowasaidia kusimamia utekelezaji wa vipaumbele vinavyotekelezwa katika maeneo yao ya utawala.
Wizara hizo zimefanya mawasilisho hayo leo Machi 17, 2023 wakati wa kikao kazi cha wakuu wa wilaya kilichofanyika Jijini Dodoma.
Hatua ya wizara hizo kuwasilisha vipaumbele hivyo ni kunatokana na maombi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI ya kutaka wakuu hao kupitishwa kwenye utekelezaji wa shughuli za wizara za kisekta ili kwenda kusimamia na kutekeleza majukumu hayo kwa weledi.
Lengo la uwezeshaji huo katika kuwajengea uwezo Wakuu wa Wilaya ili kuwawezesha kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa weledi na kuelewa mipaka na miongozo ya kusimamia wakati wanatekeleza majukumu yao.
Wizara zilizowasilisha vipaumbele ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ofisi ya Makamu ya Rais Muungano na Mazingira na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
Nyingine ni Wizara ya Nishati, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wazara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Wizara ya Mifugo na Uvuvi


