WANANCHI KARAGWE NA NZEGA WAPATIWA ELIMU YA LISHE BORA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Jumla ya wananchi 159 wa vijiji vya Omurusimbi wilayani Karagwe,Igunga wilayani Kilolo wamepatiwa elimu ya Lishe ikiwa ni maadhimisho ya siku ya afya na lishe.

Mafunzo hao yametolewa katika vijiji hivyo vya mikoa ya Kagera na Iringa ikiwa na muendelezo wa maadhimisho hayo kila baada ya miezi mitatu ambapo huduma mbalimbali za afya na lishe hutolewa kwa wananchi.

Elimu hiyo imejumuisha namna ya kuandaa na kula mlo kamili kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika vijiji vyao huku ikilenga kupunguza tatizo la utapiamlo ikiwemo udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Vile vile wananchi hao wamepatiwa elimu ya ulaji wa mlo kamili ili kuepuka utapiamlo hususan udumavu kwa watoto.

Lishe bora ni muhimu kwa afya ya binadamu na hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya Moyo,Kisukari,Shinikizo la damu,kuongeza uwezo wa mwili kufanya kazi na kuepuka tatizo la utapiamlo hasa wa mwili na akili kwa watoto chini ya miaka mitano

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)