WADAU WA ELIMU WAJADILI NJIA ENDELEVU ZA KUGHARAMIA ELIMU YA JUU NA KATI

MUUNGANO   MEDIA
0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula ametoa wito kwa wadau wa elimu ya Juu kujadili kwa kina njia bora na endelevu za ugharamiji elimu ya Juu.

Akizungumza jijini Dododma wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza kuhusu ugharamiaji wa Elimu ya Juu nchini, Dkt. Rwezimula amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipo katika mageuzi makubwa ya elimu ambayo yataongeza fursa kwa vijana wengi kujiunga na elimu ya juu na hivyo kuongeza uhitaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia masomo hayo.

Ameongeza kuwa kongamano hilo linapaswa kujadili kwa kina maandalizi ya sekta ya elimu ya juu katika kupokea ongezeko la wanafunzi wanaotokana na mikakati ya serikali ya kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ikiwemo elimo bila ada pamoja na kuangalia namna ya kugharamia wanafunzi wa vyuo vya kati.

“Kongamano hili lije na majibu juu ya namna bora ya kupata fedha ambazo zitasaidia wanafunzi wengi kusoma elimu ya juu, kwani kwa sasa hivi chanzo kikubwa ni Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, mageuzi makubwa tunayokwenda kuyafanya katika sekta ya elimu yataongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga jiunga na elimu ya juu na kati, hivyo lazima tuhakikishe tuna vyanzo mbalimbali” amesisitiza Dkt. Rwezzimula.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa kwa sasa tayari Benki ya NMB imeshaunga mkono juhudi za Serikali kwa kutenga kiasi cha shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kutoa mikopo ya elimu yenye riba ndogo, huku akitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kushiriki katika kutoa mchango wao katika kugharamia sekta ya elimu nchini bila kusahau vyuo vya kati.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Prof. Hamis Dihenga amesema kongamano hilo linalenga kuhakikisha wanajadili na kutathimin njia mbalimbali zitakazowezesha ugharamiaji wa elimu ya juu unakuwa na vyanzo vingi na endelevu badala ya kusubiri fungu kutoka serikalini pekee.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Abdul- Razaq Badru amesema Bodi hiyo inatekeleza mageuzi makubwa.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)