TUME YA MADINI YATOA ELIMU KWA WADAU WA MADINI KWENYE MAONESHO KATIKA JUKWAA LA PILI LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Leo Machi 15, 2023 Tume ya Madini imeanza kutoa elimu kupitia maonesho yanayoendelea jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya Jukwaa la Pili la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini. 

Jukwaa hilo la siku tatu linalokutanisha kampuni za madini, watoa huduma kwenye migodi na taasisi za kifedha lengo lake ni kuwakutanisha watoa huduma na kampuni za madini ili kubadilishana uzoefu, fursa zilizopo ili kufungamanisha Sekta ya Madini na sekta nyingine kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.

Taasisi nyingine chini ya Wizara zinazoshiriki ni pamoja na Taasisi ya Uhamasishaji wa Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)