NAIBU KATIBU BW. MUTATEMBWA AHIMIZA KASI UJENZI WA JENGO LA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya   Maliasili na Utalii Bw.Anderson  Mutatembwa  amemtaka Mkandarasi anayejenga Jengo Jipya la Wizara hiyo  lililopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kuongeza kasi ili Jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati uliopangwa

Ametoa wito huo leo Machi 9, 2023 wakati  alipotembelea katika Jengo hilo  kwa lengo la kujionea hatua  ilipofikia  ambapo Bw. Mutatebwa amesema kukamilika kwa Jengo hilo kutasaidia Wizara kuweza kutoa huduma kwa Wananchi katika eneo moja.

Katika hatua nyingine,  Bw.Mutatembwa ameipongeza timu nzima ya Wizara inayosimamia ujenzi wa Jengo hilo Kwa usimamizi mzuri unaoleta matokeo chanya ambapo kwa sasa hatua ya ujenzi wa Jengo hilo ni wa kuridhisha  na  linatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu aliongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali Watu,   Bi. Prisca Lwangili,  Viongozi wengine wa Menejimenti ya Wizara pamoja  na 

Uongozi wa Kampuni inayojenga jengo hilo ya LI JUN.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)