HABARI KATIKA PICHA:ZIARA YA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN JIJINI ARUSHA

0

                                   


Msafara wa Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wa Jijini Arusha wakisindikiza Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akielekea Usa River kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi, baada ya Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali, tarehe 05 Machi, 2023.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha wakati akielekea KIA baada ya Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali, tarehe 05 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wakazi Maarufu wa Arumeru Timoth Palangyo na Shedrack Palangyo  mara baada ya kuhutubia Wananchi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha tarehe 05 Machi, 2023.

                               

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Zaujia Swalehe (1) mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Usa River Mkoani Arusha. Kushoto ni Mama wa Mtoto huyo Bi. Ashura Mohamed Mkazi wa Usa River, Arumeru Mkoani Arusha tarehe 05 Machi, 2023.


Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)