DART YAJIPANGA KUANZA MATUMIZI YA MABASI YANAYOTUMIA UMEME.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Emmanuel Kawau.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki Amefungua kikao cha wadau kutoka nchi 17 za Kikanda Afrika wakijikita kujadili matumizi ya nishati safi na salama kwenye magari ili kuondoka na matumizi ya petrol na Diesel kama ilivyo sasa ambapo huchangia pakubwa katika ongezeko la hewa ya ukaa Duniani.


Akifungua mkutano huo amesema mkutano huo utakuwa chachu ya matumizi ya nishati safi  na salama katika magari na kuepuka uchafuzi wa mazingira na hali ya hewa kutokana na matumizi ya  mafuta ya petroli na Diesel

Ameongeza kuwa matumizi ya nishati mbadala ambayo ni umeme kwenye magari itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa hali ya hewa na mazingira kwa ujumla na kupunguza kadhia ya magonjwa mbalimbali kwenye jamii yanayotokana na uchafuzi huo.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede amesema mkutano huo unalenga kujadili kubadili matumizi ya mabasi na magari yanayotumia Petroleum na Diesel na kutumia nishati ya umeme katika majiji yanayoendelea katika nchi za kikanda za Afrika na kupunguza hewa ya ukaa.

Ameongeza kuwa kupitia mradi wa BRT awamu ya kwanza umesaidia kupunguza zaidi ya tani Elfu 28 za kabonidaiyoksaidi kwa mwaka na kupitia mradi mpya wa mabasi  hayo  unauhusisha mbagala na viunga vyake magari 755 yatatumia nishati rafiki wa mazingira yaani umeme na kwa kufanya hivyo wataokoa Tani laki tatu na tano kwa mwaka za hewa ya ukaa.

"Katika mradi  mpya hatutakwenda na mabasi yanayotumia Diesel tena,maana teknolojia inakwenda na sisi ni lazima kwenda na teknolojia hatuwezi kukaa tu na mambo ya kale"

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)