SHULE YA MSINGI MJIMWEMA KIGAMBONI MBIONI KUBORESHWA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Timu ya Wataalamu kutoka Benki ya Dunia, Ofisi ya Rais - TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wametembelea shule ya msingi Mjimwema iliyopo katoka Manispaa ya Kigamboni kuangalia namna ya kuboresha hali ya shule hiyo kupitia mradi wa Uboreshaji wa Elimu Msingi (BOOST).

Timu hiyo iko katika ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa kupitia mradi wa uboreshaji wa elimu Msumgi (BOOST) pamoja na ule wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.

Wakiwa katika ziara hiyo walitembelea shule ya msingi Mji Mwema na kijionea maendeleo ya wanafunzi pamoja na kubaini changamoto zinazoikumba shule hiyo ikiwa ni pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu. 

Akizungumza katika ziara hiyo Mratibu msaidizi wa mradi wa Boost kutoka Tamisemi REUBEN SWILLA  amesema lengo la kufika katika shule hiyo ni kujionea hali ya miundombinu idadi ya wanafunzi na mahitaji na kuona namna mradi wa Boost unavyoweza kutatua changamoto hizo.

Alisema kutokana na wingi wa idadi ya wanafunzi katika shule hiyo kupitia mradi wa Boost Ilajengea shule mpya ya msingi itakayoweza kuchukia  baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kuwa katika mazingira rafiki zaidi ya kujufunzia.

Naye Diwani wa kata ya Mji Mwema OMARY NGULANGWA ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati za huduma za jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wamekwisha pata eneo ambayo shule mpya ya Msingi inaweza kujengwa itakayosaidia kupunguza idadi ya wanafunzi katika shule Mama ya Mji Mwema na pia kuchukua wanafunzi wanaotoka upande wa pili ambao hulazimika kuvuka barabara kubwa  ili kufikia shule kitu ambacho sio salama sana kwa watoto. 

Mratibu Elimu msaidizi kutoka Tamisemi ROBART MSIGWA amesema lengo la Serikali ni kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia hivyo waliyobaini katika shule hiyo yatajadiliwa katika mpango kazi wa Mradi wa Boost kuona namna ya kuzitatua kwa wakati.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)