Na Emmanuel Kawau.
Askofu wa kanisa la Pentekoste life house Prof Rejoice Ndalima amempongeza Rais Dkt samia suluhu kwa uongozi wake usio na tabaka kwa makundi yote ya wa Tanzania.
Hayo ameyasema jijini Dar es salaam ikiwa ni Maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani Askofu ndalima amesema Rais Dkt Samia amekuwa kiongozi wa mfano kwa kufanyakazi nzuri ya kufungua uchumi wa nchi na uhusiano kitaifa na kimataifa.
"Rais Dkt Samia katika kilele cha siku ya wanawake duniani amealikwa na umoja wa wanawake wa chadema na amekubali mwariko huo na pia amekuwa akishiriki katika shughuli mbalimbali ambazo kwa wengine wasingeweza kufanya hivyo,hivyo samia ameonyesha yeye ni mama wa wote kwa kitendo hicho cha kutobagua watu"
Aidha Askofu Prof Ndalima amewapongeza wanawake wote kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kujenga familia na taifa kwa ujumla kwa kuwaleta pamoja wanajamii wote kwa upendo wao na malezi yao mema .
"Nitoe wito kwa jamii kuacha vitendo vya kikatili kwa wanawake na kutambua kuwa wanawake ni nguzo muhimu kwenye jamii"
Prof Ndalima amesitiza wazazi na walezi kutambua kuwa wanawajibu wa kulea na kuwafundisha maadili mema watoto wao ,kuwafundisha kazi za nyumbani na si kuwaachia wasaidizi wa kazi za nyumbani.
"kila tabia inaanzia nyumbani mtoto kuanzia umri wa miaka miwili mpaka miaka kumi anatakiwa kufundishwa maadili mema na mahusiano mema na jamii yake,kupitia siku hii ya wanawake dunia tuelekeze nguvu zetu na juhudi za makusudi kwenye malezi,pia turudie zama za zamani mtoto ni wa jamii nzima sio wa mtu mmoja".
