WAZIRI KAIRUKI ALETA MATUMAINI KWA WAKAZI WA KIVULE

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na Angela Msimbira DAR-ES-SALAAM.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amesema Serikali kupitia mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar-es Salaam (DMDP) itajenga barabara ya Banana- Kitunda – Msogola yenye urefu wa kilometa 11.5 ili kuwapunguzia kadhia wakazi wa kata ya Kivule, Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kivule katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Jimbo la Ukonga, Waziri Kairuki amesema kuwa Serikali iliamua kutenga fedha kidogo kidogo kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo na fedha za Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) ilijenga barabara yenye urefu wa kilometa 2.2.

“Serikali tuliendelea kuona umuhimu wa kuitengea fedha kidogokidogo na tukijikita zaidi katika ukarabati wa maeneo korofi lakini bado tunajua haitoshelezi tunajua kuna umuhimu mkubwa wa kuweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine.”

 “Kubwa hapa nimekuja kuwahakikishia kuwa Serikali inajenga barabara hiyo, hivyo msimzonge mbunge kwa kuwa majibu tayari yapo kuwa itajengwa yote kwa ukamilifu wake,” amesisitiza Waziri Kairuki.

Amesema usanifu utaanza kupitia mradi wa DMDP na unategemewa kukamilika ifikapo Agosti, 2023 hivyo bajeti itawekwa kwa ukamilifu.

Kuhusu Shule ya Msingi Kivule, Waziri Kairuki amesema Serikali kupitia mradi wa kuimarisha elimu ya awali na msingi (BOOST) itajenga shule mpya ili kupunguza kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kwenye shule hiyo lengo likiwa ni kutokuwa na shule inayozidi wanafunzi zaidi ya 1500.

Akizungumzia barabara inayokwenda Hospitali ya Wilaya ya Kivule, Waziri Kairuki amesema barabara hiyo itajengwa kupitia mradi wa DMDP lengo likiwa ni kupunguza kadhia ya barabara kwa wananchi.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)