Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani Bi.Savera Salvatory akizungumza katika ufungaji wa hafla ya kutembelea mradi wa Afya Tek na Usimamizi Shirikishi juu ya Masuala ya Afya katika halmashauri na Manispaa ya Kibaha .Kiongozi wa Mradi wa Afya –Tek Dkt.Angel Dillip ikiwa ni katika hafla ya majumuisho mara baada ya kutembelea mradi wa Afya Tek na Usimamizi Shirikishi juu ya Masuala ya Afya katika halmashauri na Manispaa ya Kibaha.
Mtaalam Mshauri wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka shirika lisilo la kiserikali la Apotheker kupitia Mradi wa Afya Tek Dkt.Suleiman Kimata akiteta Jambo katika katika hafla ya majumuisho mara baada ya kutembelea mradi wa Afya Tek na Usimamizi Shirikishi juu ya Masuala ya Afya katika halmashauri na Manispaa ya Kibaha.
Picha ya washiriki mbalimbali katika hafla ya majumuisho mara baada ya kutembelea mradi wa Afya Tek na Usimamizi Shirikishi juu ya Masuala ya Afya katika halmashauri na Manispaa ya Kibaha.
Washiriki mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Afya,Baraza la Famasi Tanzania,watumishi wa Afya -Tek ,Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Ofisi ya Katibu Tawala pamoja na watumishi wengine sekta ya Afya kwa Ujumla wakiwa katika picha ya Pamoja katika hafla ya majumuisho mara baada ya kutembelea mradi wa Afya Tek na Usimamizi Shirikishi juu ya Masuala ya Afya katika halmashauri na Manispaa ya Kibaha.
Na.Faustine
Gimu,Elimu ya Afya kwa Umma,Wizara ya Afya.
Rai
imetolewa kwa wadau sekta ya Afya kuungana pamoja pindi wanapotekeleza miradi
ya Afya ngazi ya jamii ili kuweza kutoa huduma bora na zenye ufanisi.
Rai hiyo
imetolewa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
na Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani Bi.Savera Salvatory katika hafla ya
majumuisho mara baada ya kutembelea mradi wa Afya Tek na Usimamizi Shirikishi juu ya Masuala ya Afya katika halmashauri na
Manispaa ya Kibaha.
Bi.Savera amesema kuna wadau wengi wanaofanya kazi kwa
kushirikiana na Serikali hivyo ni muhimu kuona namna ya kuwaunganisha pamoja
huku akiupongeza mradi wa Afya –Tek kwa kuwa
mwarobaini katika kutatua changamoto za afya katika jamii kwa
halmashauri ya Kibaha na Manispaa ya Kibaha na kuongeza kuwa ni muhimu kuona
namna ya kutoa motisha ili kuwezesha kufanya kazi kwa weledi huku akizungumzia
umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote.
“Kuna wadau
wengi wanaofanya masuala ya Afya tuone
tunawajumuishaje hawa wadau ili kuweza ni namna gani ya kutoa motisha kwa
wanaotoa huduma ngazi ya jamii na katika
Bima ya Afya kwa Wote vichwani mwetu tuanze kutambua manufaa yake na tuendelee
kuelimisha jamii “amesema.
Afisa
Programu ,Elimu ya Afya kwa Umma,Wizara ya Afya Simon Nzilibili ametoa wito kwa
wadau sekta ya Afya kuendelea
kushirikiana katika uimarishaji wa utoaji huduma za Afya ngazi ya jamii.
“Wadau tukiendelea kushirikiana tutaendelea kuboresha huduma za afya ngazi ya
jamii na hii itakuwa na matokeo chanya hasa katika uimarishaji wa mifumo”amesema.
Kiongozi wa
Mradi wa Afya –Tek Dkt.Angel Dillip amesema mradi huo umeweza kufikia jamii kwa
asilimia 91.
“Tumeweza kuwafikia watu laki mbili
na elfu thelathini sawa na asilimia 91
katika maeneo haya mawili halmashuri ya Kibaha na Manispaa ya Kibaha na Afya
Tek ipo sambamba kabisa kwa kushirikiana na serikali kuelekea Bima ya Afya kwa
Wote kwani huduma ya afya -Tek inamfikia
mpokea huduma (mgonjwa)moja kwa moja akiwa nyumbani kwa njia ya teknolojia ya
kidijitali hawa watoa huduma ngazi ya jamii wamepewa hizo simu za kisasa katika
utekelezaji wa majukumu yao”amesema.
Naye Mganga
Mkuu Mkoa wa Pwani Dkt.Gunini Kamba amesema mradi wa Afya Tek umesaidia kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto
wachanga huku Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Elimu ya Afya kwa
Umma,Wizara ya Afya Erick Msunyaro
akisema mradi huo umesaidia kupunguza gharama ya utumiaji wa karatasi
Ikumbukwe
kuwa Mradi wa Afya-Tek unatekelezwa katika Halmashauri ya Kibaha na Manispaa ya
Kibaha lengo likiwa ni kuchangia kupunguza vifo vya wajawazito,mama
waliojifungua, na watoto chini ya miaka mitano na kuboresha afya za vijana
balehe ambapo unatekelezwa kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya,TAMISEMI,Baraza la Famasi,Timu za Afya za Mkoa
na Halmashauri na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Apotheker na D-tree International .
Hivyo,mradi
huu hutumia mfumo wa teknolojia ya kidijitali kuwaunganisha watoa huduma za
afya katika ngazi ya jamii(WAJA),wahudumu wa maduka ya dawa muhimu(DLDM) na
vituo vya huduma za afya na umeanza
kutumika kuanzia Julai 2020 na hadi sasa
umeunganisha watoa huduma ngazi ya Jamii 240,DLDM 149, vituo vya kutolea huduma
za afya vya umma 39 na binafsi 10 .
Pia ,mradi
huu ulitoa mafunzo kwa watumiaji wa mfumo takribani 500 ,vitendea kazi ikiwemo simu za mkononi
450 zenye mfumo wa Afya Tek.
MWISHO.











