TAMISEMI YASHIRIKI KIKAO CHA 9 CHA KAMATI KUU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi, Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza kikao cha tisa cha Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye Kituo cha Mikutano JNICC, jijini Dares Salaam, leo Februari 25, 2023.

kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ambao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Aidha, Ofisi ya Rais TAMISEMI imewakikishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange aliyeambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe.

Pamoja na Mambo mengine, Kamati kuu imepokea na kujadili Mgawanyiko wa idadi ya watu katika maeneo ya utawala, Idadi ya watu katika Majimbo ya uchaguzi kwa Tanzania na utekelezaji wa mpangokazi wa Mwongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeoa ya Sensa ya Watu na Makazi 2022.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)