IDARA YA UTALII YATAKIWA KUJIONGEZA KUTANGAZA UTALII NDANI NA NJE YA NCHI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, katika mfululizo wa kukutana na Idara na Vitengo vya Utalii katika wizara hiyo, leo Jumamosi amekutana na Idara ya Utalii katika ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma. 

Idara hiyo ina dhamana ya maendeleo na utangazaji wa utalii ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali hasa Bodi ya Utalii (TTB) na hata wadau wengine wa sekta binafsi. 

“Kazi hapa imefanyika lakini lazima sasa mikakati yetu ya kutangaza utalii isiwe ya kinyonge kama tena kuandaa kalenda, tshirt na vitu vidogo kama hivyo pekee; twende viwango vya Royal Tour ambayo Mhe Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan alijitoa akawekeza fedha na muda wake ndio leo inatulipa kwa watalii kumiminika hapa nchini,” alisema Dkt. Abbasi. 

Mbali ya kuitisha kikao cha pamoja cha kimkakati mwezi ujao kati ya Idara hiyo na Bodi ya Utalii, Dkt. Abbasi pia amewataka watendaji wa Idara hiyo kujipanga na kujiongeza ipasavyo kwani katika siku zijazo Wizara hiyo na nchi kwa ujumla inakwenda kutekeleza mkakati mkubwa sana wa kuitangaza nchi na vivutio vyake kama ilivyokuwa kwa uwekezaji wa viwango vya Royal Tour.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)