MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE LAZIMA UKAMILIKE ILI WATANZANIA WANUFAIKE.

0

 


Na.Faustine Gimu ,

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa wasiwasi kwa watanzania kuwa Muswada sheria ya   Bima ya Afya kwa Wote lazima serikali itahakikisha inasimamia unapitiwa na kukamilika ili kila Mtanzania apate matibabu kwa Uhakika.

Msigwa amebainisha hayo leo Februari 7,2023 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Idara ya Habari ,Maelezo ikiwa ni moja ya taratibu ya idara hiyo kukutanisha wanahabari na taasisi za serikali kuelezea masuala mbalimbali yanayofanywa na serikali.

Msigwa amesema Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote una unyeti wake hivyo ni muhimu ufanyike kwa uharaka.

“Muswada  Sheria ya   Bima ya Afya kwa Wote utawasilishwa kwani una unyeti wake ,Wabunge waupitie kwa umakini kama dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya  Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hili jambo lazima lipitiwe na kukamilika haraka ili watanzania waweze kupata matibabu na umepita nafasi ya kupitiwa na sisi kama serikali hatupendi kulichelewesha jambo hili”amesema.

Aidha, Msemaji Mkuu huyo wa Serikali amesema maandalizi yote yamekamilika na kutoa wito kwa wadau  kuendelea kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa wananchi ili waelewe umuhimu wake.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)