Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) chenye lengo la kiuhimiza uwajibikaji kwa watendajii wa wakala hiyo.
Mhe. Jenista amesema pamoja na kuitaka TGFA kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa karakana ya ndege jijini Dar es Salaam kwa wakati, kuna haja ya kujenga karakana nyingine jijini Dodoma ambapo ujenzi huo unapaswa kwenda sambamba na ujenzi wa ofisi ya TGFA makao makuu jijini humo.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa, ujenzi wa ofisi ya Wakala ya Ndege za Serikali na karakana ya ndege jijini Dodoma unalenga kuunga mkono nia na azma ya Serikali ya kuhamia Dodoma, hivyo ameisitiza menejimenti ya wakala hiyo kuhakikisha inafanya jitihada za kuanza ujenzi haraka iwezekanavyo.
“Tuna kila sababu kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kuomba fedha za ujenzi wa karakana ya ndege na makao makuu ya ofisi ya TGFA jijini Dodoma kwa lengo la kuongeza ufanisi kiutendaji na kuunga mkono azma ya Serikali ya kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mradi wa ujenzi wa karakana ya ndege jijini Dar es Salaam ni mradi pekee unaotekelezwa na Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) ambao ujenzi wake ukikamilika kwa wakati utaiwezesha wakala kupata sehemu salama ya kufanyia matengenezo ya ndege zinazotumika kuwahudumia viongozi wakuu wa kitaifa


