MBIO ZA BENKI YA CRDB,SANAA YA KUJITOLEA ISIYO YA MFANO

MUUNGANO   MEDIA
0

Toleo la tatu la mbio za benki ya CRDB zilifanyika katika viwanja vya Greeens, Oysterbay Dar Es Salaam zilihitimishwa tarehe 14 Agosti mwaka 2022 kwa namna ya kipekee.

Mbio hizi zinazofanyika kila mwaka ni sehemu muhimu ya mkakati wa benki wa kurudisha kwa jamii zinazoizunguka na kukutanisha na wadau mbalimbali kutoka ulimwenguni kote.

Tofauti na matoleo yaliyopita, mbio za mwaka huu zimekusanya zaidi ya washiriki 6200 waliokimbia kati ya km5, km10, km21, km42 na km65.

Licha ya kuvutia washiriki wa kutosha hadi kufikia 6200, uwepo wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango aliyekuwa mgeni rasmi pamoja na uwepo wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya kikwete ambaye ni kati ya waanzilishi wa mbio hizo, ilipamba mbio hizo.

Akiongea baada ya kuzikabidhi taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na CCBRT kiasi cha fedha kilichopatikana kutokana na mbio hizo, Makamu wa Rais, Dkt. Mpango alisema benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za kifedha na misaada ya kijamii.“Nimefurahishwa na maamuzi ya benki ya CRDB kutumia mbio za mwaka huu kuchangisha fedha kwa ajili ya wanawake wajawazito walio katika hatari kuweza kupata huduma sahii katika hospitali ya CCBRT.” alisema Dkt. Mpango.

Alisema zaidi ya kutengeneza nafasi za ajira , biashara na ujasiriamali kupitia mbio hizi, benki ya CRDB imefanikiwa kutoa kiasi cha shillingi bilioni moja za kitanzania kusaidia wananchi wa kipato cha chini kupata matibabu katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

Mbio hizi zinaruhusu serikali kushirikiana na wadau mbalimbali, taasisi na sekta binafsi katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazohusu kufikisha huduma za kijamii nchini, aliongeza.

Mkurugenzi wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela washiriki wote waliojitokeza kuungana nao katika kufanikisha mbio hizi mwaka huu.

Nsekela aliongeza kuwa toleo la kwanza la mbio hizi lililozinduliwa mwaka 2020 lilikuwa na mafanikio makubwa na ilisaidia kutambulika duniani na Kipimo cha Utambulisho cha Riadha (Athletic Identity Measurement Scale AIMS) na World Athletics. 

“Hii ni fahari kubwa si kwa benki yetu tu bali kwa nchi yetu.”Aliongeza kuwa kama benki inayoongoza nchini, CRDB inatambua kuwa ina jukumu la kushiriki katika kusaidia juhudi za serikali katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii yetu.

Matoleo mawili yaliyopita yalijikita katika kuweka tabasamu katika nyuso za watoto wetu waliohitaji matibabu ya matatizo ya moyo, lakini mwaka huu tukasema hakuna mtoto bila mama.”Mwaka huu tumeamua kusaidia juhudi za hospitali ya CCBRT katika kuwezesha matibabu ya wanawake wajawazito walio katika hatari za kiafya

Aliongeza kuwa kiasi kilichopatikana katika mbio hizi kitatumika pia katika kukamilisha kampeni ya mazingira ya ‘Pendezesha Tanzania’Pia, kiasi kingine kitaelekezwa katika kusaidia mbio za boti kama moja ya juhudi za kutangaza utamaduni na kuvutia utalii, aliongeza Nsekela.

Zaidi ya hayo, Nsekela alieleza kuwa kwa toleo la tatu la mbio hizi, dhumuni lilikuwa kukusanya fedha na kulipia huduma za upasuaji wa moyo kwa zaidi ya watoto 100 katika taasisi ya JKCI kwa shilingi millioni 250 za kitanzania ambazo zimefanikiwa.

Dhumuni la pili lilikuwa ni kulipia kina mama wajawazito 100 wenye ujauzito ulio katika hatari kupata huduma kwa shilingi milioni 220 za kitanzania, jambo ambalo limefanikiwa pia.

Alielezea kuwa , kwa ujumla benki imeweka sera ya uwekezaji wa kudumu katika jamii inayoelekeza asilimia moja ya faida inayopatikana na benki kwa mwaka kuchangia maendeleo ya jamii yetu, hasa katika sekta za afya, elimu, mazingira, na uwezeshaji wa wanawake na vijana.

Licha ya kusaidia jamii, mbio za kimataifa ni jukwaa la wanariadha kuonyesha vipaji vyao na kuonekana duniani kote ambako mbio hzi zinatazamwa.

Alisema pia zawadi zilizotolewa katika mbio hizi zinaonyesha namna benki hii inasimamia michezo hasa ya riadha nchini.Kama haitoshi, aliongeza kuwa hii ni nafasi ya jamii kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya miili yao, hasa katika kipindi hiki ambapo magonjwa yasiyoambukizwa yanapoongezeka.“Nawapongeza wote waliowezesha kuweka tabasamu katika nyuso za watoto wenye magonjwa ya moyo wanaohudumiwa JKCI na kina mama wenye ujauzito ulio katika hatari wanaohudumiwa CCBRT.

Mwisho, ningependa kuwapongeza washiriki wote kuongoza katika mbio hizi. Nawaachia salamu za pekee za mbio hizi zisemazo Mbio za Benki ya CRDB, Kasi Isambazayo Tabasamu”, alisema Nsekela.“Nimekimbia mbio kadhaa na mara nyingi zilizokuwa na ladha tofauti, lakini kwenye mbio hizi nimezipenda kwani nimeweza kutoa na kupokea tabasamu na kuwapungia washiriki wengine ndani ya tisheti zao za Kasi Isambazayo Tabasamu”, alisema

 Joseph Munywoki , mshindi wa mbio za kilometa 42 upande wa wanaume.“Mbio za benki ya CRDB ni tukio linaloleta hamasa kushiriki, ushindi huu uwaendee watoto wote wanaohitaji huduma za upasuaji wa moyo, Mungu awalinde na awaponye”, alisema Agnes Ngolo, mshindi wa mbio za kilometa 21 upande wa waawake, akiwa na tabasamu mwanana.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)