Afisa
Programu ,Elimu ya Afya kwa Umma,Wizara ya Afya Simon Nzilibili akizungumza katika hafla ya
kutembelea mradi wa Afya Tek na
Usimamizi Shirikishi juu ya Masuala ya
Afya katika halmashauri na Manispaa ya Kibaha.
Kiongozi wa Mradi wa Afya –Tek Dkt.Angel Dillip akiwasilisha mada namna wanavyotekeleza mradi wa Afya -Tek katika halmashauri na Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani.
Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania Elizabeth Shekalaghe akichangia mada katika kikao cha mradi wa Afya -Tek Kibaha Pwani.
Afisa Ufuatiiaji na Tathmini Elimu ya Afya kwa Umma ,Idara ya Kinga ,Wizara ya Afya Erick Msunyaro akichangia mada katika kikao cha mradi wa Afya -Tek Kibaha Pwani.
Afisa Tehama Elimu ya Afya kwa Umma ,Idara ya Kinga ,Wizara ya Afya Victor Kisila akiwa katika kikao cha mradi wa Afya -Tek Kibaha Pwani.
Na.Faustine
Gimu,Elimu ya Afya kwa Umma,Wizara ya Afya.
Katika
kuelekea sheria ya Bima ya Afya kwa Wote,wadau wa sekta ya Afya wameaswa kushirikiana
na Serikali uimarishaji wa mifumo katika kuhakikisha kila mwananchi anapata
huduma bora za afya.
Hayo
yamebainishwa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na Afisa Programu ,Elimu ya Afya kwa
Umma,Wizara ya Afya Simon Nzilibili katika hafla ya kutembelea mradi wa Afya Tek na Usimamizi
Shirikishi juu ya Masuala ya Afya katika
halmashauri na Manispaa ya Kibaha.
“Tunapoelekea Bima ya Afya kwa Wote,tunatoa wito wadau wetu
wanaotekeleza mradi wa Afya –Tek wawe tayari ,pale inapotokea serikali inahitisha
wadau mbalimbali walio na utaalam kwenye
matumizi ya mifumo tuweze kushirikiana
kwa pamoja ili kuboresha na itarahisisha wananchi kunufaika zaidi na Bima ya
Afya kwa Wote kupitia Mifumo iliyo imara”amesema.
Katika hatua
nyingine Nzilibili ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
kwa kuwa mstari wa mbele katika usimamizi kuhakikisha Elimu ya Afya kwa Umma
inamfikia kila mtu hususan elimu katika
kuelekea Bima ya Afya kwa Wote na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana na
wadau katika uimarishaji wa huduma za Afya.
Kiongozi wa
Mradi wa Afya –Tek Dkt.Angel Dillip amesema lengo kuu la Mradi wa Afya-Tek ni
kusaidia kuboresha afya ya mama,mtoto na vijana balehe ambapo hadi sasa
wameshafikiwa wanajamii 230,000 sawa na asilimia 92% ya idadi ya wanajamii wote
katika halmashuri ya Wilaya ya Kibaha na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.
“Tumefikia wanajamii laki mbili na
elfu thelathini(230,000]sawa na asilimia 92% na faida za Afya –Tek imeweza
kupunguza kuchelewa kuhudumia wagonjwa na mgonjwa anapofika zahanati au kituo
cha Afya ufuatiliaji unafanyika kwa uharaka na kuweza kupata huduma kwani kabla
ya Afya –Tek kulikuwa na njia za utumiaji wa karatasi na ilikuwa vigumu
kufuatilia wagonjwa kwamba wamefika
kituo cha afya au la lakini kwa kutumia mfumo wa Afya-Tek huduma inafanyika kwa
uharaka na Mgonjwa anapata huduma”amesema.
Mganga Mkuu
Halmashauri ya Kibaha Mkoani Pwani Dkt.Wilford Kondo amesema mradi wa Afya-Tek
umeweza kusaidia kupunguza kutoka vifo 8
vya mama wajawazito mwaka 2021 hadi kifo
kimoja kwa mwaka 2022 huku mwaka huu hakuna kifo kilichoripotiwa katika
halmashauri hiyo huku mwakilishi Baraza la Famasi Kibaha Wilbard Semvua akisema mfumo wa Afya Tek
unarahisisha mgonjwa kupata huduma kwa wakati.
Mtoa huduma
wa duka la dawa Muhimu Daima Gada pamoja na mtoa huduma ya Afya ngazi ya jamii
kata ya Kongowe Simen Rashid wamesema Afya –Tek imerahishisha kuokoa muda pindi
wanapotoa huduma na kuibua changamoto zinazotokea.
Ikumbukwe
kuwa Mradi wa Afya-Tek unatekelezwa katika Halmashauri ya Kibaha na Manispaa ya
Kibaha lengo likiwa ni kuchangia kupunguza vifo vya wajawazito,mama
waliojifungua, na watoto chini ya miaka mitano na kuboresha afya za vijana
balehe ambapo unatekelezwa kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya,TAMISEMI,Baraza la Famasi,Timu za Afya za Mkoa
na Halmashauri na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Apotheker na D-tree International .
Hivyo,mradi
huu hutumia mfumo wa teknolojia ya kidijitali kuwaunganisha watoa huduma za
afya katika ngazi ya jamii(WAJA),wahudumu wa maduka ya dawa muhimu(DLDM) na
vituo vya huduma za afya na umeanza
kutumika kuanzia Julai 2020 na hadi sasa
umeunganisha watoa huduma ngazi ya Jamii 240,DLDM 149, vituo vya kutolea huduma
za afya vya umma 39 na binafsi 10 .
Pia ,mradi
huu ulitoa mafunzo kwa watumiaji wa mfumo takribani 500 ,vitendea kazi ikiwemo simu za mkononi
450 zenye mfumo wa Afya Tek.
MWISHO.
