Na Gideon Gregory, Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dkt. Tumaini Gurumo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefungua milango ya kupata mikopo kwa wanafunzi wa chuo hicho kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania Bara na Visiwani.
Kauli hiyo ameitoa leo Februari 9,2023 Jijini Dodoma mbele ya vyombo vya habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Chuo hicho katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita ambapo amesema mwaka 2021/2022 wanafunzi zaidi ya 850 walipata mkopo kulinganisha na wanafunzi 1705 walipata mkopo kwa mwaka 2022/2023 ikiwa ni zaidi ya nusu ya waliopata mkopo wamepata kwa asilimia 100%.
Amesema chuo hicho kinatoa elimu na mafunzo ya ubaharia kuanzia madaraja ya usaidizi (Ratings) hadi madaraja ya juu ya maofisa wa melini kwa upande wa uongozaji meli au unahodha na uhandisi wa mitambo ya meli (Master Mariner na Chief Marine Engineer).
“Awali, mafunzo haya yalikuwa yakikomea daraja la nne na la tatu la maofisa wa vyombo vya usafiri majini, ilipofika mwaka 2003 ndipo DMI ilipata hadhi ya kutoa mafunzo ya Ubaharia hadi madaraja ya juu. “Hadhi hii ilipatikana baada ya Serikali kuwekeza kwa nguvu katika kusomesha wakufunzi na kununua vifaa na mitambo ya kufundishia kulingana na matakwa ya Mkataba wa STCW, 1978 unaosimamiwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO),”amesema.
Dkt. Gurumo ameongeza kuwa Chuo hicho kinafanya tafiti na kutoa ushauri elekezi kwa Serikali na taasisi binafsi.
“Baadhi ya shughuli zinazofanywa ni usanifu na uandaaji wa michoro ya vyombo vya usafiri majini, stability testing, inclination and tonnage testing na tathmini ya njia za vyombo vya majini katika vyanzo vya maji, baadhi ya vyombo ambavyo DMI imevipatia huduma ni MV Kigamboni, MV. SAR IV, MV. MozMV. Mbeya, MV. Tawa na MV. Mafia AmbulanA
Amesema vifaa vya uokozi katika usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji ni nyenzo muhimu kwa usalama wa watu na mali zao, pia amesema DMI inafanya shughuli za ukarabati kwa weledi na uaminifu kwa meli za Tanzania na za kigeni pia zinapofanya safari zake nchini.

