Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Taasisi ya Kupambana
na Kuzuia Rushwa nchini[TAKUKURU] Mkoa wa Dodoma imeanzisha kampeni maalum ya
uelimishaji kwa jamii dhidi ya madhara
ya rushwa ijulikanayo "ULIPO
TWAJA" ambayo uwafuata wananchi waliopo kwenye mikusanyiko na kuwaelimisha
masuala ya ubadhilifu na rushwa ambapo hadi sasa wananchi takribani 45,000
wameelimishwa kwenye mikusanyiko 88 ndani ya mkoa wa Dodoma .
Amesema hiyo ni katika
utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan ambapo aliagiza TAKUKURU ijikite Zaidi kuzuia ubadhilifu kabla
haujatokea katika miradi ya maendeleo.
“Tunawafuata wananchi
kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo
Amesema mkoa wa Dodoma
unakadiriwa kuwa na wakazi 2,729,153 na kwamujibu wa sensa ya watu na makazi ya
mwaka 2012 asilimia 52.2 ya watanzania ni wale wa rika la miaka 15 hadi 64
hivyo katika kampeni hiyo ya ULIPO TWAJA Takukuru Mkoa wa Dodoma imekusudia
kuwafikia angalau asilimia 10 ya wananchi wa rika hilo ambao ni takribani
wakazi 142,461.
Ameeleza kuwa wao kama
Taasisi ya kuzuia na kupamabana na rushwa wameona uelimishaji huo ni sahihi
kwani utawafikia wananchi wanatumia muda mwingi katika shughuli za kujipatia
riziki zao masokoni,Vituo vya bajaji na bodaboda vijiwe vya kahawa au wale
ambao wanaenda kupata huduma kama mikusanyiko ya wanufaika wa TASAF, siku za
lishe kwenye Vituo vya afya, siku za kliniki au chanjo,stendi za daladala na
mabasi,Nk.
"Lengo la kampeni
hii ni kuwafikia wananchi ambao kulingana na aina ya kazi au Biashara
wanazofanya sio rahisi kuwapata kwenye mikutano ya hadhara au mikutano mingine
rasmi kama ya Vijiji na Mitaa inafahamika wazi wengine uendeshaji wa maisha yao
hutegemea uwepo wao katika maeneo hayo yamikusanyiko hivyo sio rahisi kuondoka
na kuacha shughuli zao ili wahudhurie mikutano ya hadhara ,"amesema
Kibwengo.
Aidha amesema
iwapo mkusanyiko husika utakuwepo saa 12 asubuhi basi ULIPO TWAJA
itawafuata na kuwaelimisha hata kama mkusanyiko huo utakuwa mchana au
njioni .
Akiwa katika eneo la uelimishaji soko la Bonanza
jijini Dodoma Afisa Uchunguzi Dawati la Elimu kwa Umma TAKUKURU Sabeth Mshana amesema katika kuelekea siku ya
wanawake Duniani Machi,8,2022 wameamua kujikita Zaidi kuelimisha wanawake juu
ya manyanyaso wanayopata ikiwemo rushwa ya ngono huku Mkuu wa uelimishaji
TAKUKURU mkoa wa Dodoma Faustine Malecha akiwataka wanawake kuwa majasiri katika
mapambano ya rushwa.
Akizungumza baada ya kupata elimu hiyo ya Rushwa
,mmoja wa wafanyabiashara jijini Dodoma Belice Malima amesema elimu ya rushwa
ina umuhimu mkubwa katika jamii