VITA VYA UKRAINE NA URUSI KUISABABISHIA TANZANIA HASARA YA TSH.BILIONI 30 KILA MWEZI

0



 

Na.Mwandishi wetu,Dodoma.

 Kutokana na Serikali kuondoa tozo ya Sh100 kwa kila lita ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa miezi mitatu kuanzia mwezi Machi,serikali itapunguza mapato bilioni 30 kwa kila mwezi yatokanayo na nishati ya mafuta .

 Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Meneja Mawasiliano na  Uhusiano Mamlaka ya   udhibiti wa huduma  za Nishati na Maji[EWURA]Titus Kaguo wakati

akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukomo wa bei ya nishati ya mafuta kuanzia Machi,22022 ambapo amesema kuondoa tozo ya Tsh.100 kila mwezi kwa nishati ya mafuta imesababishwa na sababu mbalimbali zinazoweza kuchochea kupaa kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, ikiwemo vita vya UKRAINE na URUSI.

Kuondoa tozo hiyo ya Tsh.100 itawaletea unafuu kidogo watanzania huku serikali ikipata hasara huku akitangaza pia kupanda kwa nishati hiyo ambapo kwa bandari ya Dar Es Salaam ,Mwezi Machi bei za rejareja na dizeli na petrol zimeongezeka kwa Tsh.60 kwa lita sawa na asilimia 2.42 na Tsh. 65 kwa lita sawa na asilimia 2.77 huku bei za rejareja za mafuta ya taa zikipungua kwa Tsh.83 kwa lita sawa na asilimia 3.63.

Ikumbukwe kuwa , Jumatatu Februari 28, 2022 Wizara ya Nishati

ilitoa taarifa ya kuondoa tozo ya Tsh.100 huku sababu za kuondoa tozo hiyo ya Tsh.100 ni kutokana na kuendelea kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia kunakosababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine. Taarifa hiyo imesema kuwa Waziri wa Nishati, January Makamba ameidhinisha na kusaini marekebisho ya kanuni inayohusika na Tozo hiyo ili kutimiza uamuzi huu wa Serikali.

 

 

 

 

 

 

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)