Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kutokana na
ugonjwa wa homa ya manjano kuripotiwa nchini Kenya Machi,3,2022 katika Kaunti ya Isiolo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika
la Afya Duniani [WHO]. Wizara ya Afya imetoa tahadhari kwa wananchi kujikinga
na ugonjwa huo.
Hayo
yamesemwa leo Machi 9,2022 na waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dodoma amesema
kuna tetesi zingine kutokea nchini Uganda hivyo wizara ya Afya imejipanga
kudhibiti ugonjwa huo ambapo baada ya uchunguzi wa wizara bado ugonjwa
haujaingia nchini .
Waziri Ummy ameanisha miongoni mwa dalili za ugonjwa wa
homa ya manjano kuwa ni pamoja na kutokwa damu puani,kuumwa na kichwa.
AidhaWaziri
Ummy ametaja nchi barani Afrika zilizo hatari kukumbwa na wimbi la
ugonjwa wa homa ya manjano kuwa ni pamoja na Angola, Benin ,Burkina faso
,Burundi,Cameroon,Jamhuri ya Afrika ya kati,Chad,Ivory Coast DRC Congo ,Guine
Ikweta ,Gabon,Gambia,Guine,Guine Bissau,Kenya ,Liberia
.Mali,Mauritania,Niger,Nigeria,Rwanda,Senegal,Sierra Leone ,Sudan
Kusini,Togo,na Uganda.
Hata
hivyo,ameanisha mikakati ya Wizara katika mapambano ya ugonjwa huo ni pamoja na
kuchanja kwa wasafiri ambapo kwa nchi za Afrika mashariki gharama za chanjo ni
Tsh.30,00 huku akiagiza wataalam wa afya kwenda mipakani katika kuhakikisha mtu
anayeingia nchini kutoka nchi zenye
idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa huo wanachanjwa homa ya manjano.
Mwakilishi Mkaazi wa shirika la Afya Duniani [WHO]Dkt.Tigest Katsela
Mangestu amesema asilimia 60 ya wagonjwa wa homa ya manjano hufariki
dunia huku akibainisha sababu za kuitwa homa ya manjano ni kutokana mwili pamoja na macho kuwa na rangi ya njano.
Ikumbukwe kuwa ,katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania
haijawahi kuwa na taarifa ya mgonjwa yeyote aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa
Homa ya Manjano tangu mwaka 1950