Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma ,
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ameiagiza
halmashauri ya Wilaya ya Bahi kufuta andiko la ujenzi wa kituo cha mabasi kwa
Tsh.Milioni 20 kwani kiasi hicho
akiendani na hadhi ya halmashauri .
Mtaka amebainisha hayo Wilayani Bahi katika mwendelezo
wa ziara yake kuhusu maelekezo ya Rais
ukamilishaji anwani za makazi na posti kodi,kuhamasisha kiwango cha ufaulu
pamoja na kuinua kiwango cha uchumi kwa kuibua miradi mbalimbali bunifu ya
maendeleo .
Mkuu huyo wa mkoa amesema Bahi ndio lango kuu la
Kuingilia makao makuu jijini Dodoma hivyo haiwezekani kujenga kituo cha mabasi kwa kiwango cha chini cha
Tsh.Milioni 20
“Milioni 20 stendi ya kwa hadhi ya Bahi,Milioni 20 ni stendi ya kata moja kubwa,Bahi ndio Gateway ya Makao makuu ,Bahi ndio Kibaha ya Dar Es Salaam tunataka kuona Mbezi kama Kimara Mwisho,PHD ,Degree mnakaa mnakubaliana kujenga stendi ya Tsh.milioni 20 mtachekwa hadi na mbwa”alisisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Aidha,Mkuu huyo wa Mkoa amesema haiwezekani Wilaya ya
Bahi iwe na maeneo mazuri ya kilimo halafu wananchi wake wawe masikini na
tegemeo katika mikoa jirani hivyo ameagiza Februari ,28,2022 kukutana na skimu zote 16 za umwagiliaji katika kuleta mapinduzi ya kilimo huku pia
akiagiza kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi na kumtaka mkurugenzi wa Bahi kwenda kujifunza Kahama jinsi maeneo
ya kimkakati yalivyopangwa.
Kuhusu suala la elimu ,Mkuu wa Wilaya ya Bahi
Mwanahamis Mkunda amesema wilaya yake imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha
kiwango cha ufaulu kinaongezeka.
Nao baadhi ya Madiwani kutoka kata za Wilaya ya Bahi akiwemo
Blandina Magawa diwani wa Ibugule,Anthony Lyamunza diwani wa Makanda pamoja na
Sosthenes Mpandu diwani wa Mpamantwa wamesema watahakikisha wanashirikiana
na Watumishi wa Halmashauri katika
kuchangia mawazo chanya kwa maendeleo ya Bahi
Akiwa ziara katika halmashauri ya Kondoa Mjini mkuu huyo
wa Mkoa alikutana na makundi mbalimbali ya watumishi wa halmashauri na
kusikiliza kero zao akiwemo Afisa Ugavi halmashauri ya Kondoa Mjini kutokuwa na
maelewano mazuri na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Paul Sweya.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka aliwataka watumishi wa
halmashauri ya Kondoa Mjini kuacha mivutano na badala yake wawe
na mshikamano na kuwa wabunifu kwa kuibua miradi bunifu
na ya kimkakati itakayosaidia kuleta maendeleo na kuvutia
wawekezaji.
“Mnagombana kwa sababu hamna ajenda ,mkurugenzi kata nane
unashindwa kupanga mipango madhubuti inakuwa halmashauri ya mfano,unaweza
ukaamua
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa
mji Mohammed Kiberenge anaahidi kuitisha kikao cha dharura cha baraza la
madiwani kusuluhisha mgogoro huo baina ya Mkurugenzi na Afisa Ugavi.
Katika hatua nyingine Mtaka aliziagiza halmashauri kuja na
mkakati wa kutunga sheria ndogo zitakazosaidia kuwabana watu waharibifu wa
miundombinu ya anwani za makazi na postikodi
Mtaka alitoa maagizo hayo
wakati akizindua zoezi la uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi na
postikodi katika barabara ya Iboni halmashauri ya Kondoa .
Mkuu huyo wa Mkoa alisema haiwezekani serikali kuwekeza fedha
nyingi katika utekelezaji wa mifumo ya anwani za makazi na postikodi halafu
ajitokeze mtu kuharibu miundombinu kwa kuuza kama chuma chakavu.
Akizungumzia katika utekelezaji wa zoezi la mfumo wa
anwani za makazi na postikodi ,mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kondoa Paul
Sweya amesema jumla ya barabara 255 zilibainishwa kwa kupewa majina
ambapo halmashauri imeandaa mabomba 230,na vibao 255 vya mitaa huku mkuu
wa Wilaya ya Kondoa ,Dkt.Khamis Mkanachi akisema zawadi kwa Rais ni kukamilisha
zoezi hilo mapema kabla ya muda uliopangwa ambao ni Mei,2022.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka alitembelea
shule ya wasichana Kondoa katika kuhamasisha suala la elimu.
Mtaka amezitaka
kamati za taaluma mkoani Dodoma kukaa pamoja kuwaandaa vyema wanafunzi walio
kwenye madarasa yenye mitihani ya kitaifa ili kuwaandaa kufanya vyema wanafunzi
katika mitihani yao.
Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza kuwa Kila ufaulu wa A,kwa
matokeo kidato cha sita Ofisi ya mkoa itagharamia kwa Tsh.Elfu
thelathini[30,000],na shule itakayoingia 10 bora itapewa milioni 5 huku kila A
kwa matokeo kidato cha nne itagharamiwa Tsh.20,000.
Hivyo aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidi kwa manufaa yao
wenyewe na serikali imewekeza gharama kubwa katika shule hiyo.