Katika taarifa fupi iliyotolewa na msemaji wake mjini New York Marekani baada ya mazungumzo hayo Guterres amweleza rais Zelenskyy dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kuimarisha msaada wa kibinadamu kwa watu wa Ukraine.
Na katika hilo amemwambia Rais wa Ukraine kwamba “ Jumanne ijayo Umoja wa Mataifa utazindua ombi la fedha kwa ajili ya operesheni zetu za kibinadamu nchini Ukraine.”
Kwa mujibu wa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 150,000 wamefungasha virago na kuikimbia Ukraine huku idadi hiyo ikirtarajiwa kuongezeka na wengine kwa maelfu wametwanywa katika ameneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Na wote hao Umoja wa Mataifa unasema wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu, ikiwemo maji, malazi, chakula na huduma za afya.
Chanzo:Radio Umoja wa Mataifa