JUMAA AWESO NAINBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:PICHA KUTOKA MAKTABA
Wizara ya maji na umwagiliaji yatoa shilingi milioni mia moja ili kuongeza chachu ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Kakola halmashauri ya Msalala.
TEASER MAJI………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo afanya uteuzi wa mabalozi wawili.
NA,
Ethiopia yapitisha sheria inayopiga marufuku wageni kuasili watoto raia wa nchi hiyo.
TAARIFA HII YA HABARI INASOMWA NAMI…………..
BRIDGE……………
Wizara ya maji na umwagiliaji imetoa shilingi milioni Mia moja ili kuongeza chachu ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kakola halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga ,Naibu waziri wa wizara ya maji,Jumaa Aweso amesema kuwa Fedha hizo ni kutokana na ombi la Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige hali ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya maji.
Hata hivyo Naibu waziri huyo amewatahadharisha wakandarasi wa maji kusimamia ipasavyo mradi huo wa maji na si kwa kufanya mazoea ya kuchelewesha.
Awali mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige amebainisha kuwa tatizo la maji katika kijiji cha Kakola ni changamoto kubwa ambapo ndoo moja inauzwa kwa shilingi 1000 tangu miaka ya 2009.
Mradi mkubwa wa Maji Kakola utatumia jumla ya Tsh.bilioni 14 na Ziara ya Naibu waziri wa Maji Juma Aweso inaendelea katika manispaa ya Shinyanga.