Wakazi wanne mjini Kahama leo wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kahama kwa tuhuma ya kujiwakilisha kama watumishi wa serikali na kujipatia fedha kwa njia udanganyifu.
Watuhumiwa hao ni Paul Kayanda[36} mkazi wa Majengo ,Shaban Njia [26] mkazi wa Nyahanga,Simon Dioniz [42] na Raymond Mihayo[42] Mihayo wote wanatuhumiwa kwa madai ya kujiwakilisha kama watumishi wa serikali maafisa wa usalama wa taifa na kujipatia fedha kiasi cha shilingi milioni moja kutoka kwa mkazi mmoja mkazi wa Banhi wilayni Kahama.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Keneth Mtembei ,mwendesha mashtaka Zuberi Mateso wamedai kuwa watuhumiwa walikamatwa na jeshi la polisi Januari 9 mwaka huu nyumbani kwa Jane Mbeshi [46] mganga wa jadi kwa kumtuhumu kufanya ramli chonganishi na kudai awape fedha hizo.
Washtakiwa hao ambao wanadaiwa kuwa waandishi wa habari kutoka mjini Kahama wamekana mashtaka yote mawili na kurudishwa rumande kwa kukosa dhamana hadi Januari 24 mwaka huu shauri lao litakapotajwa tena.
Kamanada wa polisi mkoani Shinyanga Simon Haule amesema kuwa Shaban Njia,Raymond Mihayo,Paulo Kayanda na Simon Dioniz na mwingine George Maziku ambaye bado anatafutwa na Jeshi la Polisi hilo Januari 6 Mwaka huu walijiwasilisha kwa Mbeshi na kudai kuwa ni maafisa Usalama wa Taifa na kudai wapatiwe pesa.