MAIGE ATOA MIFUKO 50 YA SARUJI KUSAIDIA UJENZI WA ZAHANATI NYAMISHIGA MSALALA KAHAMA

0
Image result for mh ezekiel maige

Mbunge wa Msalala,Ezekiel Magolyo Maige

Mbunge wa jimbo la Msalala wilayani Kahama  mkoani Shinyanga Ezekiel Maige ameahidi  kutoa mifuko 50 ya saruji katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyamishiga kata ya Lungunya halmashauri ya Msalala.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho Maige amesema kuwa msaada huo alioutoa   ni kuunga mkono juhudi  za wananchi katika shughuli za maendeleo.


Hata hivyo Maige ameagiza kuorodheshwa dawa zote zinazotakiwa kutolewa katika vituo vya afya  ili wananchi waweze kufahamu kwani kuna baadhi ya dawa hutolewa bure  na kutokufahami hilo watumishi wa afya hutumia mianya hiyo kuuza dawa zilizotolewa ruzuku na serikali ili ziwanufaishe wananchi.

Aidha Mbunge huyo amewataka wananchi kukata bima ya CHF iliyoboreshwa ili wapate Bima kwa ajili ya matibabu kwa gharama nafuu,  huku akiwataka wazee pia  wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea kujiandikisha ili nao waweze kupata bima bure.

Katika hatua nyingine Mmoja wa wakunga wa jadi wa kijiji cha Nyamishiga Selema Ndelembi amelalamikia suala la wakunga kijijini hapo kutolipwa  licha ya kazi kubwa wanazofanya  za kuwasaidia akina mama wajawazito kuwapeleka hospitalini  kujingufungua .

Akilitolea ufafanuzi suala hilo diwani wa kata ya Lunguya Benedict Musa Manuary amesema kuwa suala la wakunga wa jadi ni uzembe na  ukiritimba wa watumishi wa Afya  akiwemo mganga wa kituo cha Afya cha Lunguya  na kuongeza kuwa wakunga wanmekuwa na mchango mkubwa wa kuokoa uhai wa wajawazito wanaojifungulia majumbani hata nyakati za usiku.

Ziara ya Mbunge Maige  imeanza leo katika kata ya Lunguya ambapo amefanya mikutano miwili ya hadhara katika vijiji vya Nyamishiga na Madaho katika  halmashauri ya Msalala.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)