Wakazi wa
kijiji cha Buyozi kata ya Mwakata halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga wamelalamikia ubovu wa miundo mbinu ya barabara ya Buyozi Mwakata hususan
kipindi hiki cha masika.
Wakizungumza
na Gimu Blog spot kijijini hapo baadhi ya wakazi
hao wamesema kuwa ubovu wa barabara hiyo kimekuwa ni kikwazo cha kukwamisha shughuli
mbalimbali za maendeleo.
Hivyo
wameiomba serikali kusaidia kukarabati barabara hiyo kwa kuweka changalawi na
kuongeza madaraja kutokana na eneo kubwa la barabara hiyo kuwa la mbuga.
Kwa upande
wake Diwani wa kata ya Mwakata Ibrahim
Six Masanja amewataka wananchi
wa Buyozi kuwa na subira kwani tayari kuna mkandarasi ameshapatikana kupitia
wakala wa barabara vijijini na mtaani TARURA
Na.Faustine Gimua Chanzo:Mahojiano.