Idara ya
wanawake ya Dorikas Kanisa la waadventista wasabato Malunga wilayani Kahama
mkoani Shinyanga imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wafungwa katika gereza la Kahama vyenye
thamani ya Zaidi ya Sh.Laki 3.
Akizungumza
na GIMU BLOG mara baada ya kumalizika
utoaji wa msaada huo,mkuu wa Idara ya
Dorikas Kanisa la waadventista wasabato Malunga mjini Kahama Veronica Lameck amesema kuwa vitu
vilivyotolewa ni nguo ,sabuni ,mafuta na
miswaki vyenye thamani ya shilingi laki 3 na 85 elfu na 100.
.
Mzee wa
kanisa la waadventista wasabato Malunga Manase Alphonce ametoa wito kwa waumini
na viongozi kutoka taasisi mbalimbali kuwa
na moyo wa kuendelea kutoa misaada kwa wahitaji.
Naye mmoja
wa waumini wa kanisa la waadventista wasabato Malunga Christina Lukwalo amesema
kuwa ni wajibu wa kila mtu kuwasaidia
watu wenye uhitaji maalum ikiwa ni pamoja na wafungwa,wajane,yatima na
wazee na kuacha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwatenga.
Kwa upande
wake Kaimu mkuu ambaye pia ni mrakibu wa
gereza la wilaya ya Kahama Lusana Shigumha amelipongeza kanisa hilo kwa
kuwajali wafungwa huku akizitaka taasisi zingine kufanya hivyo.
Utoaji wa wa
misaada kwa watu wenye uhitaji maalum ni moja ya kipaumbele kikuu kinachofanywa na kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni
pote kama maagizo ya yesu kristo
yasemavyo kuwasaidia wafungwa ni jambo la
busara.