:RUZUKU
Baraza la madiwani
halmashauri ya Msalala wilayani Kahama
mkoani Shinyanga limeomba serikali kuu kuziingiza kwenye mfumo wa ruzuku shule
za bweni ambazo hazimo kwenye mfumo huo
ili kuondoa mkanganyiko wa kuchangia chakula shule hizo.
Wakizungumza katika
kikao cha baraza hilo,Mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Mibako Mabubu na diwani wa kata ya Ikinda Matrida Musoma
wamesema kuwa kati ya shule 5 za mabweni
ni shule moja tu inayopewa ruzuku na serikali huku zingine ni
makubaliano na wazazi.
Makubaliano ya
wazazi kuchangia chakula shuleni
yanatokana na shule hizo kuwa mbali hivyo waliamua kufanya hivyo ili kuzuia
mimba shuleni kutokana kutembea umbali mrefu.
Aidha wameongeza kuwa
ili kuondoa mkanganyiko huo ni vyema serikali ikaziingiza kwenye mfumo wa
ruzuku shule zote 5 za sekondari za
bweni zilizopo katika halmashauri hiyo na kama haina uwezo iendelee kuruhusu
michango.
Shule za sekondari ambazo zipo kwenye mfumo wa bweni lakini hazimo kwenye mfumo wa ruzuku ni Chela,lunguya,busangi na Isaka
na Shule iliyo kwenye mfumo wa ruzuku ni Mwalimu Nyerere huku Ntobo
na Bulige zikiwa katika hatua ya
Mwisho ya ukamilishaji na kuwa za bweni.
Katika hatua nyingine
mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala
Mibako Mabubu ameitaka Wakala
wa barabara vijijini TARURA kuwa karibu na
halmashauri hiyo ili kufanyakazi kwa ufanisi zaidi