Jumla ya vijana 12 wanaoishi katika mazingira hatarishi mjini Kahama wameamua kuacha matendo maovu na kuanza kuhudhuria kwenye nyumba ya ibaada katika kanisa la waadventista wasabato Kahama mjini.
Wakizungumzia juu ya kubadilika tabia na kuachana na matendo maovu wakiwa kanisani hapo vijana hao wamesema kuwa maisha yao hapo awali yalikuwa ni utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na wizi .
Mmoja wa wazee wa kanisa la wasabato Kahama Mjini Wilson Peter amesema kuwa vijana hao wameendelea kupokea wito na kubadilika kuwa na matendo mazuri.
Naye mmoja wa vijana Sabato Mwita ambaye kwa sasa anaishi katika maisha mazuri Sabato Mwita amewatia moyo vijana kuendelea kubadilika kwani naye alipitia maisha hatarishi ya mtaani lakini imebaki kuwa historia .
Licha ya kanisa la waadventista wasabato Kahama mjini kupokea vijana 12 waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya limeshiriki meza ya bwana ambapo mmoja wa wazee wa kanisa hilo Petrol Kakenele amesema kuwa meza ya bwana humuweka mtu karibu na Mungu na pia ni kielelezo cha ushirika na yesu Kristo.