MAKAMBI YA VIJANA KATIKA KANISA LA WASABATO YAHITIMISHWA MONDO KAHAMA

0

Wazazi na walezi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameaswa  kuwa makini katika malezi ya watoto wao ili waweze kuishi  katika makuzi mazuri  na yenye mienendo yenye maadili mema.

Hayo yamesemwa leo na mchungaji wa kanisa la waadentista wasabato Kagongwa Mch.Emanuel Magai katika hitimisho la mkutano wa makambi kwa vijana wilayani Kahama yaliyofanyika katika shule ya Msingi Mondo halmashauri ya mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

Magai amesema kuwa ni heri mzazi ama mlezi kumlea mtoto katika njia nzuri impasayo kwani itakuwa msingi bora wa maisha yake na kumwepusha katika mambo maovu.


Kwa upande wao  meneja wa kambi hilo Hezron Malembeka na Mwalimu wa vijana hao  Severino Patrick  wamezungumzia juu ya mkutano huo jinsi mafunzo yalivyotolewa


Nao baadhi ya vijana waliohudhuria katika mkutano huo wa makambi ya vijana wamesema kuwa mafunzo hao yamewasaidia katika uelewa juu ya Utoaji wa huduma ya kwanza katika jamii.

Jumla ya vijana 150 wamehitimisha makambi hayo ya vijana na neno kuu lilikuwa ni biblia na bibila pekee.
MWISHO.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)