Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu sita wakiwemo
raia wanne wa China kwa kosa la kusafirisha na kuhifadhi mawe
yanayosadikiwa kuwa na madini kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule
watuhumiwa walikamatwa Disemba 6,2017 saa saba mchana katika kata ya
Ibadakuli wilaya ya Shinyanga na askari wa usalama barabarani wakati
wakikagua roli lenye namba za usajili T 209 AVH lililokuwa limebeba mawe
hayo yaliyochongwa mfano wa virungu.
Kamanda Haule alisema baada ya kuwakamata wachina hao na madereva wao,
walisema mawe hayo wanayapeleka kuyahifadhi kwenye kwenye kiwanda cha
kutengeneza mafuta ya kula cha Jielong Tz Co . Ltd kilichopo mjini
Shinyanga.
Raia wa China waliokamatwa ni Bai Tao 40, Chen Dunlu 33, Huanran Liu na
Jianhua Xiong na madereva wao wawili ambao ni Anwari Shabani na Joseph
Kapoli.
Mmiliki wa mali hizo Huanran Liu amekiri kutokuwa na lesseni wala kibali
cha kusafirisha mawe hayo na kudai yeye ni mtafiti wa madini na
ameyahifadhi kwenye kiwanda hicho cha mafuta kwa muda tu na hakuwa
tayari kutaja wapi wameyapata.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi, Hamisi
Kamando amesema kuna uwezekano mkubwa wa mawe hayo kuwa na madini ya
thamani ingawa hawezi kutaja ni aina gani hadi uchunguzi wa kimaabara
ufanyike.
Kamando amesema kitendo cha watuhumiwa hao kukutwa na mawe hayo bila
kuwa na leseni wala kibali cha kujihusisha na biashara ya madini ni
kinyume cha kifungu cha 6 cha Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na
marekebisho yake ya mwaka 2017.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa Shinyanga ACP Simon Haule akionyesha
mawe waliyoyakamata yanayosadikiwa kuwa na madini ndani yake.Picha zote na Marco Maduhu – Malunde1 blog
Kamanda Haule akimhoji Jianhua Xiong ndani ya kiwanda cha kutengeneza
mafuta ya kupikia cha Jielong kwanini wamekiuka sheria za nchi kwa
kusafirisha mawe hayo na kuyahifadhi kwenye kiwanda cha mafuta ya kula
bila kibali
Trei za mawe hayo yanayosadikiwa kuwa na madini ndani yake
Trei za mawe yanayodaiwa kuwa na madini
Trei za mawe hayo
Trei za mawe
Kamanda Haule akiwa katika gari lililokamatwa na mawe yanayosadikiwa kuwa na madini
Gari lililokamatwa na mawe yanayosadikiwa kuwa na madini lenye namba za
usajili T 209 AVH mali ya Deogratius Maganga mkazi wa Tabora.