PICHA KUTOKA MAKTABA
Jamii wilayani
kahama mkoani shinyanga imeaswa kutoa taarifa katika mamlaka husika wanapoona
vitendo vya ukatili kwa watoto vikitendeka.
Hayo yamesemwa
na mwanasheria kutoka shirika la msaada wa kisheria lililopo wilayani Kahama KAHAMA
PARALEGAL ORGANIZATION (KAPAO) Bi Upendo Erisha Mahobe wakati
akizungumza na Gimu Blog.
Amesema kuwa
kutengana kwa wazazi ni tatizo kubwa ambalo linasababisha watoto wengi kukubwa
na ukatili wa aina mbalimbali wawapo mtaani.
Aidha amesisitiza kuwa wazazi wanapotengana
baba anajukumu la kutoa mahitaji yote ya muhimu anayopaswa kupatiwa mtoto hivyo wanapaswa kufuata sheria inavyoelekeza.
Katika hatua
nyingine amewataka watoto wasifumbie macho vitendo vyote vya kikatili wanapofanyiwa kwani wanajukumu
la kutoa taarifa pia.
Pamoja na hayo
ametumia nafasi hiyo kuitaka jamii kuelewa haki za watoto na kuzijua sheria
zinazowalinda watoto wote ili kuwalinda dhidi ya ukatili katika jamii.