Taasisi ya Yatima Foundation imeandaa hafla ya chakula cha pamoja kwa watoto yatima ikiwa ni sehemu ya kuwapa faraja, matumaini na msaada katika maisha yao ya kila siku, chini ya kauli mbiu isemayo, "Sisi ni wao na wao ni sisi."
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa taasisi ya Yatima Foundation, Musa Hussein, amesema kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023, Yatima Foundation imeendelea kuwasaidia watoto waliopoteza wazazi au walezi wao kwa kuwapatia malazi, chakula, mavazi na elimu.
Aidha, amewahimiza watoto hao kutokata tamaa, akisisitiza kuwa kufiwa na wazazi si sababu ya kushindwa kufikia ndoto zao za maisha.
Baadhi ya watoto walionufaika na huduma za taasisi hiyo wametoa shukrani zao, wakisema msaada wanaoupata umewarejeshea matumaini na kuwasaidia kuendelea na masomo yao.
Kwa upande wake, mwanauchumi Hatibu Hamisi ambae ni mdau alie hudhuria katika hafla hiyo amewataka wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na yatima Foundation taasisi changa iliyo anzishwa kwa lengo la kuwa saidia watoto yatima ili kuhakikisha watoto yatima wanapata huduma stahiki na fursa za kujenga maisha bora ya baadaye.