WIZARA YA ELIMU YAOMBA KUIDHINISHIWA SHILINGI TRILIONI 2.3 KWA AJILI YA BAJETI YA 2026/2027

MUUNGANO   MEDIA
0

 



              Na Avelina Musa - DODOMA.


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 2.398 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu na miradi mbalimbali ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2026/2027.


Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.


Prof. Mkenda amesema kati ya fedha hizo, Shilingi 2,394,423,829,000 zimeombwa kwa ajili ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Fungu 46), ambapo Shilingi 697,841,881,000 ni kwa matumizi ya kawaida.


Amesema ndani ya fedha za matumizi ya kawaida, Shilingi 648,082,352,000 zitatumika kwa mishahara ya watumishi huku Shilingi 49,759,529,000 zikielekezwa kwenye matumizi mengineyo.


"Shilingi 1,696,581,948,000 zinaombwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo Shilingi 1,337,249,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 359,332,948,000 ni fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo."amesema.


Aidha amesema Wizara kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO (Fungu 18) imeomba kuidhinishiwa Shilingi 3,866,993,000 kwa matumizi ya kawaida.


 Prof. Mkenda amesema kati ya fedha hizo za UNESCO, Shilingi 1,335,020,000 ni kwa ajili ya  mishahara na Shilingi 2,531,973,000 ni kwa ajili ya matumizi mengine.






Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)